Sunday, April 19, 2009

LAKWAO TSACCOS (2008) LTD LOAN POLICY

1
Namba ya kuandikishwa . ……………………
SERA YA MIKOPO
YA
CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO
CHA
LAKWAO TALANTA
SAVINGS AND CREDIT COOPERATIVE SOCIETY (2008) LTD.
LALTA
OVADA KWAMTORO
2
YALIYOMO
YALIYOMO ...................................................................................................................................................... 2
SERA MKOPO – LAKWAO TALANT SACCOS LTD ....................................................................................... 3
UTANGULIZI. .................................................................................................................................................. 3
DIRA YA CHAMA ............................................................................................................................................ 3
AZMA/MWELEKEO WA CHAMA .................................................................................................................... 3
MADHUMUNI YA CHAMA ............................................................................................................................... 3
MISINGI NA KANINI KUU ZA UTOAJI MIKOPO. ......................................................................................... 4
SEHEMU YA I.................................................................................................................................................. 5
SIFA ZA MKOPAJI. .................................................................................................................................... 5
SEHEMU YA II ................................................................................................................................................. 5
KUSUDIO LA MKOPO NA AINA ZA MIKOPO. .......................................................................................... 5
SEHEMU YA III. .............................................................................................................................................. 6
MAOMBI YA MIKOPO. ............................................................................................................................... 6
SEHEMU YA IV................................................................................................................................................ 7
KUTATHMINI NA KUIDHINISHA MIKOPO ................................................................................................ 7
SEHEMU V ....................................................................................................................................................... 7
MAPENDEKEZO NA MAAMUZI YA MKOPO .............................................................................................. 7
SEHEMU YA VI................................................................................................................................................ 7
ADA YA MIKOPO ........................................................................................................................................ 7
SEHEMU YA VII .............................................................................................................................................. 8
DHAMANA YA MKOPO ............................................................................................................................... 8
SEHEMU YA VIII ............................................................................................................................................. 8
MKATABA WA MIKOPO .............................................................................................................................. 8
SEHEMU YA IX ................................................................................................................................................ 9
MIPANGO YA UREJESHAJI MIKOPO ........................................................................................................ 9
SEHEMU YA X ................................................................................................................................................. 9
UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA MIKOPO. ............................................................................................. 9
SEHEMU YA XI .............................................................................................................................................. 10
UKUSANYAJI MIKOPO ............................................................................................................................. 10
SEHEMU YA XII ............................................................................................................................................ 10
UCHELEWESHAJI WA MAREJESHO ....................................................................................................... 10
SEHEMU YA XIII ........................................................................................................................................... 11
KUAHIRISHA ULIPAJI WA MKOPAJI ...................................................................................................... 11
SEHEMU XIV ................................................................................................................................................. 12
KUFUTWA KWA DENI LA MKOPO .......................................................................................................... 12
SEHEMU YA XV ............................................................................................................................................ 12
BIMA........................................................................................................................................................... 12
SEHEMU YA XVI ........................................................................................................................................... 12
FORM YA MAOMBI YA MIKOPO .............................................................................................................. 12
TAARIFA ZA MWANACHAMA .................................................................................................................. 12
TAARIFA ZA MKOPO ............................................................................................................................... 12
TAARIFA ZA DHMANA NA UDHAMINI ................................................................................................... 13
UTHIBITISHO ............................................................................................................................................ 13
MAONI YA MWAJIRI ................................................................................................................................ 13
UAMUZI WA KAMATI YA MKOPO ........................................................................................................... 13
3
SERA YA MKOPO – LAKWAO TALANTA SACCOS LTD
UTANGULIZI.
LAKWAO T SACCOS LTD ni taasisi ya hiari ya kifedha inayohudumia wanachama ambao ni
wananchi wanaoishi katika vijiji vya Ndoroboni, Kwamtoro, Msera, Ilasee, Magambua, Handa,
Lahoda, Wairo, Manantu, Kisande, Dinae, Baaba, Jogolo, Takwa, Kinyamsindo, Mengu na
Ovada, Tarafa ya Kwamtoro wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma na wengine wanaotoka nje ya
maeneo haya ili mradi wakubalike katika vikundi vya eneo hili.
LAKWAO T SACCOS LTD ni chama kilichoandikishwa rasmi mwaka …….. na mrajisi wa ushirika
chini ya sheria namba 20 ya mwaka 2003. namba yake ya kuandishwa ni ………………….
DIRA YA CHAMA
Asasi ya kifedha inayoongoza katika utoaji wa huduma bora za kifedha vijijini kwa kushirikisha
wadau wote.
AZMA/MWELEKEO WA CHAMA
Kuwawezesha wanachama wengi kununua hisa, kuweka akiba na amana ili kupata mikopo yenye
Masharti na gharama nafuu ili kujilitea maendeleo endelevu.
MADHUMUNI YA CHAMA
Madhumuni ya chama hiki pamoja na mambo mengine ni:-
a) kuendeleza uanachama wa mtu mmoja na kukuza uwezo wao kiuchumi ili kuwawezesha
kujiwekea akiba, kukopa kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kurejesha kwa wakati
kupitia vikundi vyao vya wanachama kati ya 10 – 15.
b) Kupokea kiingilio, hisa, akiba na amana kutoka kwa wanachama na kutoa mikopo kwa
kuzingatia kiwango cha akiba na amana za mwanachama.
c) kujenga tabia ya kujiwekea akiba na amana na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima
miongoni mwa wanachama.
d) kuweka viwango vya riba juu ya akiba, amana na mikopo kwa wanachama vinavyokidhi
gharama za uendeshaji wa LAKWAO T SACCOS LTD.
e) kupanga utaratibu unaofaa wa kutunza na kuweka kinga ya fedha ya wanachama dhidi ya
hasara/majanga.
f) kuunda mtaji wa kutosha kuendesha shughuli za LAKWAO T SACCOS LTD.
4
g) kujenga na kuimarisha uwezo wa wanachama kuendesha na kusimamia chama kwa njia
ya Elimu ya ushirika na ushirikishwaji wa wanachama.
h) kubuni utaratibu mzuri wa kutoa taarifa za shughuli za LAKWAO T SACCOS LTD kwa
wanachama na kupokea Maombi ya wanachama wapya.
i) kununua hisa na dhamana (bond) kwenye vyombo vya fedha na serikali baada ya kufanya
utafiti wa kina na wa kitaalamu.
j) kuwawezesha wanachama kuongeza kipato katika kaya na kusaidia kuongezeka kwa
mzunguko wa fehda katika eneo lao kwa kuhakikisha kuwa huduma na mahitaji muhimu
yanapatikana kwa urahisi katika eneo la LAKWAO T SACCOS LTD.
k) kutoa elimu ya ujasiriamali, uendeshaji na usimamamizi wa biashara kwa wanachama.
l) kushirikana na taasisi nuingine za fedha na vyama vingine vya akiba na mikopo kwa ajili
ya kuongeza mtaji wa chama na kusaidiana.
m) kufanya shughuli nyingine muhimu kwa manufaa ya wanachama na ustawi wa LAKWAO T
SACCOS LTD.
MISINGI NA KANUNI KUU ZA UTOAJI MIKOPO.
Kupata faida ni dhana ambayo itasaidia kusitawi na kuendelea kwa chama. Kuwepo kwa sera hii
ya mikopo inatarajiwa kupunguza hatari za hasara zinazoweza kujitokeza katika chama. Vigezo
hivi pamoja na vifuatavyo vimewekwa ili kuwa kama kinga ya kudhibiti utendaji bora wa
huduma za taasisi yenyewe:-
a.) Ili biashara iweze kustawi, uaminifu katika biashara ni jambo muhimu sana na chama
kitalisimamia kuhakikisha kuwa wanachama wake wanakuwa waaminifu na biashara ya
kukopesha inakuwa endelevu.
b.) Chama kitatilia mkazo kuhakikisha kuwa wanachama wake wanaorejesha mkopo kwa
muda unaotakiwa wanapewa motisha. Aidha wanachama watakaoweza kukopa na
kurejesha mapema wanapatiwa nafasi ya kufikiriwa kwa mikopo mikubwa.
c.) Kuhakikisha kuwa wanachama wanajisikia kuwepo kwa mkopeshaji. Chama kupitia
watumishi wake watahakikisha kuwa wanakuwa karibu na mkopaji na kuona kuwa
urejeshaji wa mkopo unafanyika kama ilivyokubalika.
d.) Chama kitazingatia zaidi tabia ya mkopaji kama moja ya vigezo muhimu wakati wa utoaji
mkopo. Vingine ni pamoja na uwezo, dhamana, hali yake na mtiririko wa fedha.
e.) Misingi ya malipo itabakia kuwa ni uwezo wa kuzalisha kipato katika shughuli za kila siku
za mwanachama. Ili kupunguza hatari ya kupata hasara, utoaji wa mkopo utazingatia pia
uzoefu wa mkopaji na ujuzi wake katika shughuli zake za uzalishaji.
5
f.) Huduma za kifedha ni shughuli ya biashara. Usimamizi wa mikopo unajengwa na kufuata
taratibu na kutafsiri kanuni ili kuweza kuepusha matumizi mabaya ya fedha za
wanachama na kuporomoka kwa taswira na hadhi ya chama cha ushirika wa akiba na
mikopo yaani LAKWAO T SACCOS LTD.
SEHEMU YA I.
SIFA ZA MKOPAJI.
LAKWAO T SACCOS LTD kitazingatia sifa za kikatiba kwa mwanachama zinazomwezesha kuomba
na kufikiriwa kupewa mkopo. Sifa hizi ni pamoja na;
1. mwombaji awe ametimiza angalau Miezi sita tangu ajiunge na LAKWAO T SACCOS LTD
mwombaji awe angalau amenunua si chini ya hisa mbili chamani.
2. mwombaji awe ameweka akiba na/au amana kwa kiasi kinachomwezesha kupata mkopo
na kwamba Maombi ya mkopo hayatazidi mara mbili ya kiasi cha akiba na/au amana
aliyonayo chamani. Kama chama kitaweza kupata fedha nyingine kwa kuwakopesha
wanachama wake zaidi ya mara mbili, wanachama watapatiwa taratibu za kufuata.
3. mwombaji pamoja na kuwa na akiba na/au amana kwa kiasi cha kutosha chamani
anatakiwa kushiriki na kutimiza majukumu mbalimbali ya chama, hususani, kuhudhuria
mikutano ya chama na kushiriki kikamikilifu.
4. mwombaji asiwe na madeni mengine na kama yapo, pawepo na ushahidi kuwa anao
uwezo wa kuyalipa.
5. mwombaji awe na dhamana ya hakika ya kumwezesha kupata mkopo (k.m mshahara,
shughuli ya uzalishaji mali, biashara,n.k.)
SEHEMU YA II
KUSUDIO LA MKOPO NA AINA ZA MIKOPO.
LAKWAO T SACCOS LTD kitakuwa tayari kumkopesha mwanachama ambaye amenuia kuwa na
mradi wa kiuchumi au shughuli yoyote ya kihalali (kama kilimo cha kisasa, bustani za mboga,
ufugaji wa kuku, ng’ombe, nyuki, uvuvi, mazao ya misitu, viwanda vidogovidogo, biashara za
rejareja, na huduma nyingine, kama vile Elimu, afya ujenzi wa nyumba bora, kununua hisa
kwenye makampuni, n.k.
Mikopo katika ushirika wa LAKWAO T SACCOS itagawanyika katika makundi makuu yafuatayo:-
a.) Mkopo wa biashara – huu ni mkopo wa muda mfupi kwa ajili ya mtaji wa biashara
b.) Mikopo ya uzalishaji – hiii ni mikopo ya msimu kwa ajili ya wakulima kununulia
pembejeo na shughuli zingine zihusuzo kilimo
6
c.) Mikopo ya huduma - hii ni mikopo kwa ajili ya ada ya Elimu, matibabu, hifadhi ya
Chakula, harusi, hija n.k.
d.) Mikopo ya dharura- hii ni mikopo kwa ajili ya misiba, ugonjwa hasa kwa mwanachama
mwenye mkopo mingine tayari.
e.) Mikopo ya mtaji mkubwa au rasilimali – hii ni mikopo kwa ajili ya kupata mtaji wa
malighafi au kulipa vibarua/wafanyakazi au ununuzi wa rasilimali kama mashine, ardhi
Majengo, magari nk. Kwa ajili ya uzalishaji.
mikopo hii pia itatengwa katika madaraja manne (4)
i.) Mikopo midogo – kuanzia Tsh. 1 – 400,000/= itatozwa riba ya 8% kwa Miezi 6
ii.) Mikopo ya kati - kuanzia 400,001 – 2,000,000/= itatozwa riba ya asilimia 10% kwa
Miezi 12.
iii.) Mikopo mikubwa – 2,000,001/= na kuendelea, itatozwa 12% kwa Miezi 12.
iv.) Mikopo ya dharura- 20% ya amana na akiba, hii itatozwa 5% kwa miezi 3.
N.B. Mkutano mkuu unaweza kubadilisha viwango hivyo kulingana na hoja na wakati.
SEHEMU YA III.
MAOMBI YA MIKOPO.
Mwombaji wa mkopo atatakiwa kufuata taratibu zifuatazo:
1. kabla ya kupewa mkopo, mwanacham atatakiwa kujaza fomu maalumu ya Maombi ya
mkopo.
2. Pia atatakiwa kuonyesha mambo muhimu yafuatayo kwenye fomu maalumu ya Maombi ya
mkopo
a.) Jina la mwombaji
b.) Nambari ya kitabu cha akiba
c.) Kikundi anachotoka
d.) Kijiji chake
e.) Anuani ya mwombaji
f.) Aina ya mkopo
g.) Kiasi cha fedha anachoomba
h.) Sababu/madhumuni ya mkopo
i.) Muda wa marejesho ya mkopo
j.) Kiasi cha fedha kitakachorejeshwa kwa kila awamu.
k.) Dhamana ya mkopo.
l.) Ahadi ya wadhamini.
m.) Uthibitisho/kiapo juu ya ukweli wa maelezo aliyoyatoa
n.) Saini ya mwombaji
o.) Tarehe ya Maombi
7
SEHEMU YA IV
KUTATHMINI NA KUIDHINISHA MIKOPO
Mambo yafuatayo yatatakiwa kuzingatiwa na kamati ya mikopo wakati wa kutathmini Maombi ya
mikopo kabla ya kuidhinisha;
1. madhumuni ya mkopo (kwa nini mwanachama anaomba mkopo)
2. uwezo wa mwombaji wa kulipa mkopo anaouomba pamoja na riba.
3. uwezekano wa mkopo kulipwa kwa wakati uliokusudiwa
4. Kuwepo kwa chanzo/au vyanzo vingine vya mapato
5. Aina ya dhamana ya mkopo anayoitoa
6. usahihi wa maelezo aliyoyatoa kwenye fomu ya Maombi
7. Tamko la wadhamini wake
8. Aina ya mkopo
9. Tabia na mwenendo wa mkopaji
10. Mwombaji kuwa na makao maalum
SEHEMU V
MAPENDEKEZO NA MAAMUZI YA MKOPO
1) Uamuzi wa mkopo wa muda mrefu utatolewa ndani ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja toka
Maombi ya mwanachama yalipofika kwa kamati ya mikopo.
2) Maamuzi ya Maombi ya mkopo wa dharura yatatolewa baada ya kipindi kisichozidi siku tano
tangu maombi yalipofika kwa kamati ya mikopo.
3) Kiasi cha dharura kitakachotolewa kwa mwanachama aliyeomba kitakuwa si zaidi ya asilimia
ishirini ya kiasi cha akiba na amana alizonazo mwanachama chamani. Maombi ya dharura yapitie
kwenye kikundi cha mwanachama kabla ya kufikishwa kwenye kamati ya mikopo.
4) mkopo wa dharura utatolewa kwa mwanachama aliyekwisha kopa mkopo wa kawaida.
5) Endapo mkopo utakuwa nje ya kipengele Na 4. hapo juu mkopaji atahudumiwa ndani ya siku
tano lakini riba itabaki kama ilivyo katika mkopo wa kawaida.
SEHEMU YA VI
ADA YA MIKOPO
8
1) Kwa kuanzia, mkopo unaotolewa na LAKWAO T SACCOS LTD utalipiwa ada ya shilingi 1,000/=
ili kufidia gharama za utawala na mchanganuo wa mkopo, isipokuwa, chama kupitia mkutano
mkuu, kinanaweza kufikiria, kujadili na hatimaye kuweka kiwango kingine cha malipo ya ada ya
mikopo.
2) Endapo LAKWAO T SACCOS LTD kitaamua kuwa na utaratibu wa kutoza malipo ya ada ya
mikopo, ada hizo zinaweza kutofautiana kutokana na aina moja ya mkopo hadi nyingine.
SEHEMU YA VII
DHAMANA YA MKOPO
1) kila mkopo unaotolewa na LAKWAO T SACCOS LTD ni lazima uwe na dhamana yake.
2) Dhamana za mkopo zitakazokubaliwa na LAKWAO T SACCOS LTD ni pamoja na;
a.) Jinsi LAKWAO T SACCOS LTD inavyomwamini mwanachama wake katika kurejesha
madeni.
b.) Udhamini wa Mwajiri (kwa wanachama ambao ni waajiriwa) ambapo anatia saini na
kupiga muhuri kwenye fomu ya Maombi.
c.) Udhamini wa wanachama ambao ni wanakikundi wasiopungua wawili ambao dhamana zao
za akiba katika chama kwa pamoja hazitapugua nusu ya mkopo ulioombwa isipokuwa kwa
mkopo unaotokana na fedha za nje ya chama kutoka katika taasisi za kifedha ambapo
dhamana ya mkopo itatokana na makubaliano kati ya chama na taasisi husika.
SEHEMU YA VIII
MKATABA WA MIKOPO
Mkataba wa mkopo ni makubaliano ya kisheria kati ya LAKWAO T SACCOS LTD na mkopaji au
LAKWAO T SACCOS LTD na mkopeshaji. Makubaliano hayo ni kielelezo cha kwamba chama
kimemkopesha mwanachama wake au kimekopeshwa fedha na taasisi nyingine. Kwa madhumuni
haya;
1. mwombaji aliyekubaliwa kupewa mkopo atapaswa kusaini mkataba wa mkopo.
2. mambo muhimu yafuatayo yatatakiwa kuonyeshwa katika mkataba wa mkopo;
a.) nurejeshaji mkopo ambapo mkataba utaweka bayana kuhusu muda wa kurejesha,
tarehe ya kuanza marejesho na kiasi kitakacholipwa kwa kila awamu;
b.) dhamana ya mkopaji; na
c.) kiasi cha riba juu ya mkopo kitakachotozwa kwa kuzingatia aina ya mkopo.
9
Kila mkopaji atasaini nakala mbili za mkataba wa maandishi; Nakala moja itakuwa ya LAKWAO T
SACCOS LTD na nyingine atapewa mwanachama aliyekopa ili awe akielewa Masharti na taarifa
zilizomo kwenye mkataba huo hususani juu ya urejeshaji, riba, dhamana, nk.
SEHEMU YA IX
MIPANGO YA UREJESHAJI MIKOPO
1) LAKWAO T SACCOS LTD itapanga jinsi mkopaji atakavyoweza kurejesha mkopo kutokana na
shughuli ya uzalishaji au biashara anayofanya mkopaji. Kiasi cha mkopo na riba yake itakuwa
ikilipwa kwa muda/wakati uliopoangwa ambao unaweza kuwa kwa kila wiki, mwezi hadi mkopo
utakapokwisha kulipwa. Kiasi cha mkopo ulioombwa kitatolewa kutokana na mahitaji ya
mkopaji. Kwa mfano kama ni kilimo kuna kulima, kupalilia na kuvuna. Hivyo basi kila kipindi
mkopo utatolewa kulingana na mahitaji ya mkopaji badala ya kumpa mkopo wote mara moja.
2) kiasi kinachopaswa kurejeshwa kwa mwezi/Miezi kinapaswa kuwa sawa kwa muda wote. Kwa
mfano kama marejesho ya mkopo pamoja na riba kwa mwezi ni Tshs. 10,000/=, basi kila mwezi
mkopaji anapaswa kulipa hivyo na si chini ya hapo.
3) mkopo wa dharura unapaswa kurejeshwa kwa mikupuo miwili, ikijumuisha mkopo pamoja na
riba. LAKWAO T SACCOS LTD iepuke mkopo wa dharura kulipwa zaidi ya mikupuo mitatu.
Mkopaji anapokopa afahamishwe hivyo.
4) Mkopo wa dharura utakuwa 20% ya akiba na amana za mwanachama alizonazo. Marejesho ya
mkopo huo utalipwa si zaidi ya Miezi mitatu (3) na kwa kadri itakavyo amriwa na kamati ya
mkopo. Kiwango hicho cha mkopo wa dharura kitaendelea kurekebishwa kulingana na pato la
mwanachama kupitia mkutano mkuu wa chama. Marekebisho yatafanywa na kamati ya mikopo;
hii ni pamoja na riba yake.
SEHEMU YA X
UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA MIKOPO.
1) Kamati ya mikopo itahitaji kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mkopo ili kuhakikisha kuwa
mikopo ya wanachama inatumika kama ilivyokusudiwa.
10
2) Endapo kamati ya mikopo itabaini kuwa mkopo ulioidhinishwa na kutolewa kwa
mwanachama haukutumika kama ilivyokusudiwa, mojawapo ya hatua za haraka zifuatazo
zinaweza kuchukuliwa;
a.) Kamati itamwita mkopaji (mwanachama) na kutaka kupata uhakika wa jambo hilo kutoka
kwake.
b.) Endapo itabainika kuwa ni kweli mkopo huo haukutumika kama ilivyokusudiwa, kamati
inaweza kuamuru mkopaji kuurejesha mkopo huo mara moja, au
c.) Kupunguza kiasi cha fedha kinacholingana na mkopo/fedha anayodaiwa mkopaji kutoka
kwenye hesabu ya akiba yake ili kufidia kiasi hicho, au
d.) Mkopaji hatapewa nafasi ya kukopa tena hadi hapo atakapoihakikishia kamati kuwa
mkopo atakaopewa atautumia kwa busara.
e.) Mkopaji akitaka kubadilisha Malengo ya mkopo yaliyokusudiwa ni vema awasiliane na
kamati ya mikopo na kufahamisha mabadiliko hayo.
SEHEMU YA XI
UKUSANYAJI MIKOPO
LAKWAO T SACCOS LTD itakuwa na mafanikio endapo itakuwa na uwezo wa kukusanya madeni
yake kutoka kwa wakopaji ambao ni wanachama wake. Hii ni pamoja na:-
1. kama katika eneo la chama kutakuwa na chama cha ushirika na mazao, utaratibu
unaweza kuandaliwa kati ya LAKWAO T SACCOS LTD na kile chama cha mazao ili
mwanachama anayeuzia mazao katika chama hicho fedha zake zikatwe na kulipwa mara
moja katika LAKWAO T SACCOS LTD. Pia kama kuna idadi kubwa ya watumishi, kamati ya
mikopo itafanya utaratibu wa kuwa na kumbukumbu sahihi za mikopo ambazo zitakuwa
zikiwasilishwa kwa Mwajiri mapema kabla mishahara ya kila mwezi haijaandaliwa ili
kuhakikisha kuwa makato sahihi yanafanyika kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopelekwa
kwake.
2. Endapo itabainika kuwa mkopaji ana matatizo yanayomsababishia ugumu wa ulipaji wa
mkopo anaodaiwa, kamati itafikiria kumpangia tarehe ya mbele ili kumpa nafasi zaidi ya
kulipa mkopo wake.
3. Tarehe ya kutolewa mkopo inapaswa kutumika kama siku ya kwanza. Muda wa juu kabisa
wa kurejesha mkopo usiokuwa wa dharura kwa LAKWAO T SACCOS LTD ni miaka mitatu.
Iwapo mkopo utarejeshwa wote kabla ya muda wake, malipo ya riba yatabaki vilevile.
SEHEMU YA XII
UCHELEWESHAJI WA MAREJESHO
11
Urejeshaji wa mikopo uliocheleweshwa ni pale mwanachama mkopaji anaposhindwa kurejesha
mkopo siku aliyotakiwa kwa kuzingatia mkataba. Hii inaweza kuwa ni;-
 sehemu ya mkopo – yaani fungu la wiki, mwezi/Miezi n.k halikurejeshwa kwa siku ya
mkataba au
 mkopo uliokuwa urejeshwe kwa mkupuo haukurejeshwa siku ya mkataba
ucheleweshaji wowote wa mikopo utafuatiliwa na adhabu kwa mcheleweshaji. Madhara
yatokanayo na kuruhusu uchelewesho kwa chombo cha fedha ni makubwa. Hii ni pamoja na;-
 kujenga/kuambukiza tabia hii kwa wakopaji ambao ni warejeshaji wazuri;
 chama kupata adhabu ya riba ya nyongeza kama kimekopa nje;
 biashara kulega lega kutokana na wanachama kukosa imani; na
 kuwafanya wawekezaji kuchelea au kusita kuwekeza katika chama.
Kutokana na hali hiyo, adhabu zifuatazo zitachukuliwa kwa ucheleweshaji:
 Meneja kufuatilia mkopaji – siku ya tatu baada ya mkataba. Faini ya ufuatiliaji ni Tshs.
5,000/=
 Kama deni halikulipwa lote, kuwajulisha wadhamini kuwa hisa zao zitafidia deni kama
hawatahakikisha mdaiwa amelipa katika kipindi cha wiki moja;
 Kama ni mfanyakazi kumjulisha Mwajiri wake na kumtaka kufanya marejesho pamoja na
adhabu ya 10% ya salio la mkopo huo;
 Kamati inaweza kupanga adhabu nyingine kufuatana na usumbufu atakaosababisha
mkopaji; na
 Kwa yule ambaye dhamana yake ilikuwa ni mali inayohamishika au isiyohamishika, hatua
za kuzuia, mali hizo kisheria zichukuliwe mara moja.
SEHEMU YA XIII
KUAHIRISHA ULIPAJI WA MKOPAJI
1) Mkopo utaweza kuahirishwa endapo mambo yafuatayo yamebainika kumkabili mkopaji;
 Kutokea kwa janga lolote linaloweza kumfanya mkopaji (mwanachama) kushindwa
kumudu malipo ya mkopo kama vile mafuriko.
 Mkopaji kukosa kabisa uwezo wa kulipa deni kutokana na kushuka kwa uwezo wake
kifedha, hali hii yaweza kutokana na, kifo, matatizo ya kiafya, kusimamishwa/kufukuzwa
/kupunguzwa kazi n.k.
2) baada ya mkopo kuahirishwa, ulipaji wa deni kama hili unaweza kuchukuliwa hatua zifuatazo
ili kufanikisha urejeshaji;
 Kuongeza muda wa urejeshaji,
 Kupunguza kiasi cha urejeshaji deni,
12
 Kusogeza mbele muda wa kuiva kwa tarehe/muda wa marejesho,
 Kubadili tarehe ya makubaliano ya awali ya urejeshaji wa mkopo.
 Mkopaji kutoruhusiwa kukopa tena hadi hapo atakapokamilisha marejesho ya mkopo
wake.
SEHEMU XIV
KUFUTWA KWA DENI LA MKOPO
Sehemu ya deni la mkopo inaweza kufutwa endapo uanachama wa mkopaji (mwanachama)
utakoma mali alizodhamini zitauzwa katika mazingira ambayo hisa, akiba na amana zake
kutotosheleza kulipa deni linalodaiwa na chama;
1. kifo
2. wazimu uliothibitishwa na daktari
3. wadhamini wake kukumbwa na kipengele 1 na 2 hapo juu.
SEHEMU YA XV
BIMA
Ili kuepuka madhara mbalimbali yanayoweza kutokea, LAKWAO T SACCOS LTD kitawekea bima
mikopo, fedha na mali zake nyingine
SEHEMU YA XVI
FOMU YA MAOMBI YA MIKOPO
TAARIFA ZA MWANACHAMA
1. Jina la mwanachama
2. Namba ya kitabu cha akiba
3. Anuani ya mwanachama, simu, Email.
4. Jina la kikundi chake
5. Kitongoji/ Kijiji
6. kata anamoishi
TAARIFA ZA MKOPO
13
7. Aina ya mkopo
8. Ninaomba/tunaomba mkopo wa fedha kiasi cha shs. ……….. kwa maneno) ……………
9. Madhumuni ya mkopo
10. Mkopo huu nitaurejesha kwa kipindi cha Miezi . (kwa maneno) ..
11. Marejesho ya mkopo yatafanyika kwa awamu na nitalipa/tutalipa vifungu vya shs……… .
(Kwa maneno)………………………………………………………………………………………… Kwa mkupuo
mmoja/kila wiki/kilamwezi/miezi…………...pamoja na riba juu ya mkopo.
12. Sidaiwi/tunadaiwa na ……………………………….. kiasi cha shs………………. (Kwa maneno)
………………………………………………………………………………………………………………………………………..
TAARIFA ZA DHMANA NA UDHAMINI
13. Dhamana ya mkopo huu ni ……………
14. Thamani ya mali (dhamana) ni shs ………………………….. (kwa maneno)
15. Ahadi ya wadhamini:
Sisi Kwa pamoja na kila mtu kwa nafsi yake mwenyewe tunaahidi kwamba tunamdhamini
mkopaji wa mkopo huu na Endapo atashindwa kulipa sisi tutakuwa tayari kulipa deni hilo au
sehemu ya mkopo uliobaki.
Jina……………………………………………..saini…………………………..tarehe……………………………………..
Jina …………………………………………….. saini ………………………….tarehe…………………………………
Jina………………………………………………. saini………………………….tarehe………………………………….
UTHIBITISHO
Mimi/sisi …………………………………...ninathibitisha/tunathibitisha kwamba taarifa
nilizozitoa/tulizotoa ni kweli kwa kadri ninavyojua/tunavyoujua.
Saini ya mwanachama……………………………………………..tarehe ya Maombi………………………………..
MAONI YA MWAJIRI
(sehemu hii ijazwe na Mwajiri kama mwanachama ni mfanyakazi)
Mwombaji wa mkopo huu apewe/asipewe. Kwa sababu……………………..
………………………………………………………………………………………………………………………………………
Cheo ………………………………………….saini ……………………………………………...tarehe……………..
UAMUZI WA KAMATI YA MKOPO
1. Kwa ajili ya mkopo nitakaokopeshwa/tutakaokopeshwa naahidi kuurejesha kwa chama
cha akiba na mikopo cha …………………………………………………………………………..
2. Nitarejesha/tutarejesha kiasi cha shs………………………. (kwa
maneno)………………………………………………………………………………………………………………..
14
3. Fungu la kwanza litalipwa siku ya tarehe ……………………na malipo mengine yatalipwa
kila wiki/kila Miezi …………. Hadi deni lote litakapomalizika.
4. Dhamana ya mkopo huu ni ………………………………………………
5. Saini ya mkopaji jina ………………………………….. saini………………………….tarehe…………
6. Saini za wajumbe wa kamati ya mikopo
jina ……………………………………….. Saini ……………………………….. tarehe………………………
jina…………………………………….….. saini ………………………………. tarehe ……………………...
jina …………………………………………..saini ……………………………....tarehe …………………….
8. Ushahidi
Makubaliano haya yamefanyika na kushuhudiwa na wafuatao:
Jina .;…………………………………………………..
Cheo ……………………………………………………
Saini ……………………………………... Na muhuri ………………………..
Jina ………………………………………………………..
Cheo ………………………………………………..
Saini ………………………………….….. Na muhuri ………………
Tarehe …………………………………………………..

No comments: