Tuesday, May 12, 2009

PHOTOS FOR SUNFLOWERS

SERA YA AKIBA NA AMANA LAKWAO TSACCOS

1
Namba ya kuandikishwa . ……………………
SERA YA AKIBA NA AMANA
YA
CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO
CHA
LAKWAO TALANTA
SAVINGS AND CREDIT COOPERATIVE SOCIETY (2008) LTD.
LALTA
OVADA KWAMTORO
2
YALIYOMO
YALIYOMO ......................................................................................................................... 2
SERA YA AKIBA NA AMANA ............................................................................................ 3
UTANGULIZI .................................................................................................................. 3
DIRA YA CHAMA ........................................................................................................... 3
AZMA/MWELEKEO WA CHAMA .................................................................................. 3
MIPANGO YA MBELENI ................................................................................................ 3
MADHUMUNI YA CHAMA ............................................................................................. 3
SEHEMU YA 1 .................................................................................................................... 4
VYANZO VYA FEDHA ZA CHAMA ............................................................................... 4
SEHEMU YA II .................................................................................................................... 5
AINA ZA AKAUNTI ZA AKIBA NA AMANA ................................................................. 5
SEHEMU YA III ................................................................................................................... 5
UTARATIBU WA KUPOKEA AKIBA NA AMANA ........................................................ 5
a) Akiba na amana za wanachama .................................................................. 5
SEHEMU YA IV................................................................................................................... 6
AKIBA NA AMANA KUTUMIKA KAMA KIGEZO NA DHAMANA YA MIKOPO ......... 6
SEHEMU YA V .................................................................................................................... 6
MUDA WA KUWEKA AKIBA NA AMANA .................................................................... 6
SEHEMU YA VI................................................................................................................... 7
KUCHUKUA NA KUREJESHA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA ................... 7
SEHEMU YA VII ................................................................................................................. 7
USALAMA WA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA ............................................ 7
SEHEMU YA VIII ................................................................................................................ 8
RIBA JUU YA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA ............................................. 8
3
SERA YA AKIBA NA AMANA
LAKWAO T SACCOS(2008) LTD
UTANGULIZI
Sera ya akiba na amana ni mwongozo ulioandaliwa na chama cha ushirika wa
Akiba na mikopo (LAKWAO T SACCOS LTD) kwa ajili ya uwekaji akiba na amana
za wanachama na wateja wake.
Talanta chama cha ushirika cha Akiba na mikopo (LAKWAO T SACCOS LTD) ni
asasi ya hiari ya kifedha inayowahudumia wanachama na wateja
wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi katika tarafa ya
Kwamtoro. Makao makuu ya chama yapo katika kijiji cha Ovada.
LAKWAO T SACCOS LTD imeandikishwa kama chama cha ushirika wa akiba na
mikopo chini ya sheria ya ushirika na. 20 ya mwaka 2003 na imeandikishwa kwa
Na ………………………...
DIRA YA CHAMA
Asasi ya kifedha inayoongoza katika utoaji wa huduma bora za kifedha vijijini
kwa kushirikisha wadau wote.
AZMA/MWELEKEO WA CHAMA
Kuwawezesha wanachama wengi kununua hisa, kuweka akiba na amana ili
kupata mikopo yenye masharti na gharama nafuu ili kujieletea maendeleo
endelevu.
MIPANGO YA MBELENI
a) kuhamasisha na kuelimisha jamii kujiunga na LAKWAO T SACCOS LTD
b) kushirikiana na asasi nyingine za kifedha za ndani na nje ya nchi
c) kuajiri watumishi wenye uelewa pevu juu ya ushirika wa akiba na mikopo
ili watoe huduma bora na endelevu kwa wanachama na wasio
wanachama.
MADHUMUNI YA CHAMA
Madhumuni ya LAKWAO T SACCOS LTD pamoja na mambo mengine ni:-
(a) kuendeleza uanachama wa mtu mmoja mmoja na kukuza uwezo wao
kiuchumi ili kuwawezesha kujiwekea akiba, kukopa kwa ajili ya shughuli
za kiuchumi na kurejesha kwa wakati kupitia vikundi vyao vya
wanachama 10-15.
(b) Kupokea kiingilio, hisa, akiba na amana kutoka kwa wanachama na
kutoa mikopo kwa kuzingatia kiwango cha akiba na amana za
mwanachama.
(c) Kujenga tabia ya kujiwekea akiba na amana na kuepuka matumizi
yasiyo ya lazima miongoni mwa wanachama.
4
(d) Kuweka viwango vya riba juu ya akiba, amana na mikopo kwa
wanachama dhidi ya hasara/majanga.
(e) Kuunda mtaji wa kutosha kuendesha shughuli za LAKWAO T SACCOS
LTD.
(f) Kujenga na kuimarisha uwezo wa wanachama kuendesha na kusimamia
chama kwa njia ya elimu ya ushirika na ushirikishwaji wa wanachama.
(g) Kubuni utaratibu mzuri wa kutoa taarifa za shughuli za LAKWAO T
SACCOS LTD kwa wanachama na kupokea maombi ya wanachama
wapya.
(h) Kununua hisa na dhamana (bond) kwenye vyombo vya fedha na serikali
baada ya kufanya utafiti wa kina wa kitaalamu.
(i) Kuwawezesha wanachama kuongeza kipato katika kaya na kusaidia
kuongeza mzunguko wa fedha katika eneo lao kwa kuhakikisha kuwa
huduma na mahitaji muhimu yanapatikana kwa urahisi katika eneo la
LAKWAO T SACCOS LTD.
(j) Kutoa elimu ya ujasiriamali na uendeshaji na usimamizi wa biashara
kwa wanachama.
(k) Kushirikiana na taasisi nyingine za fedha na vyama vingine vya akiba na
mikopo kwa ajili kuongeza mtaji wa chama cha kusaidiana.
(l) Kufanya shughuli nyingine muhimu kwa manufaa ya wanachama na
ustawi wa LAKWAO T SACCOS LTD.
SEHEMU YA 1
VYANZO VYA FEDHA ZA CHAMA
LAKWAO T SACCOS LTD inatarajia kupata fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli
zake, kuwekeza kwenye vitega uchumi na kutoa mikopo kwa wanachama
kutoka vyanzo vifuatavyo:-
a) Viingilio vya wanachama
b) Hisa za wanachama
c) Akiba za wanachama
d) Amana za wanachama na wateja
e) Faida kutoka Benki
f) Mikopo kutoka taasisi zingine
g) Adhabu/faini
h) Misaada au zawadi au ruzuku
i) Akiba na malimbikizo ya lazima
j) Faida kutoka vitega uchumi kama vile gawiwo (dividend) kutoka
makampuni mbalimbali ambako LAKWAO T SACCOS LTD imenunua
hisa/imewekeza.
k) Riba kutoka mikopo ya wanachama
l) Riba zitokanazo na kuhifadhi amana za wateja
m) Viingilio vya wanachama
5
SEHEMU YA II
AINA ZA AKAUNTI ZA AKIBA NA AMANA
LAKWAO T SACCOS LTD itaendesha aina tofauti za akaunti ya akiba na amana
kama ifuatavyo:-
a) Akaunti za akiba
i) Akaunti ya akiba ya lazima kwa ajili ya kujenga fungu la
kukopeshana.
ii) Akaunti ya akiba kwa ajili ya elimu ya watoto
b) Akaunti za amana
i) Akaunti ya amana ya kawaida kwa ajili ya matumizi ya kila siku
ya mwanachama au mteja
ii) Akaunti ya amana ya muda maalum (muda unaweza ukawa ni
wa miezi kadhaa (sita) au miaka kadhaa (mf. Miwili)
SEHEMU YA III
UTARATIBU WA KUPOKEA AKIBA NA AMANA
a) Akiba na amana za wanachama
i.) kuweka akiba katika LAKWAO T SACCOS LTD ni jambo la lazima
kwa kila mwanachama. Kila mwanachama wa LAKWAO T SACCOS
LTD ni lazima ajenge tabia ya kuweka akiba mara kwa mara ili
kujenga fungu la kukopeshana kama ilivyo katika masharti.
ii.) Mwanachama anaweza kuweka amana katika LAKWAO T SACCOS
LTD.
iii.) Akiba na amana zitalipwa kwa fedha taslimu tu na sio vinginevyo
iv.) Fedha za mwanachama zinaweza kupelekwa/kuwekwa na mwenye
akaunti yeye mwenyewe au mweka hazina wa kikundi chake au
kiongozi yeyote wa kikundi chake au mtu yeyote atakeyekuwa
ameaminiwa na mwenye fedha.
v.) Mweka hazina wa LAKWAO T SACCOS LTD ni lazima aandike
stakabadhi ya fedha mara tu akishapokea fedha za mwanachama
akifuatiwa na maingizo katika vitabu na kumbukumbu nyingine za
fedha kulingana na mfumo wa uhasibu uliopo.
b) Amana za wateja
Wasio wanachama (wateja) wanaweza kuweka amana zao katika
LAKWAO T SACCOS LTD kwa kulipia gharama kidogo. LAKWAO T SACCOS
LTD inaweza kupokea amana kutoka kwa makundi mbalimbali kama
vile:-
6
i) Wafanyabiashara wanaokuja kununua mifugo au mazao kwa
kuhifadhi fedha zao na kuchukua kidogo kidogo kulingana na
mahitaji yao ya kibiashara
ii) Taasisi zinazokuja kuendesha mafunzo au semina wanaweza
kuhifadhi fedha zao kwa usalama kwa muda katika chama.
iii) Wananchi wa kawaida na/ au taasisi zilizomo ndani na/au nje
ya eneo la chama.
Mteja anayekuja kuweka fedha zake katika LAKWAO T SACCOS LTD atatozwa
ada ya asilimia moja (1%) ya kiasi cha fedha kilichowekwa kwa kipindi cha
mwezi mmoja. Baada ya muda/kipindi hicho kupita ada yake itakuwa nusu ya
asilimia (0.5%) ya kiasi cha fedha kilichobaki.
SEHEMU YA IV
AKIBA NA AMANA KUTUMIKA KAMA KIGEZO NA DHAMANA YA MIKOPO
a.) Akiba na Amana za wanachama wa LAKWAO T SACCOS LTD zitatumika
kama kigezo na dhamana ya mikopo.
b.) Mwanachama ataruhusiwa kukopa mara mbili ya kiasi cha akiba na
amana alizonazo chamani wakati wa kuomba mkopo.
c.) Amana za mwanachama zinapotumika kama dhamana ya mkopo
hazitaruhusiwa kuchukuliwa hadi pale mkopaji atakaporejesha mkopo
aliopewa pamoja na riba yake.
d.) Kiasi chochote cha akiba na amana alizonazo mwanachama
kitamwezesha kuomba mkopo.
SEHEMU YA V
MUDA WA KUWEKA AKIBA NA AMANA
a.) Mwanachama wa LAKWAO T SACCOS LTD ataweka akiba na amana wakati
wowote wa mwaka kulingana na hali ya mapato.
b.) Mwanachama ataweka kiasi chochote kile kwenye akaunti yake ya akiba.
Hata hivyo mwanachama anashauriwa kuweka kiasi kisichopungua
asilimia kumi (10%) ya mapato yake anayopata kwa vipindi tofauti.
7
SEHEMU YA VI
KUCHUKUA NA KUREJESHA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA
Mwanachama wa LAKWAO T SACCOS LTD atarejeshewa au kuchukua akiba zake
endapo:-
a) Ataamua kujitoa
b) Atahama eneo la chama
c) Atafukuzwa uanachama
d) Atathibitika kuwa ni mwenda wazimu (mwanachama aliyepata na
kuthibitika kuwa ni mwendawazimu anaweza kurejeshewa haki zake au
kukabidhiwa kwa mtu yeyote atakayeteuliwa naye kumiliki haki zake
kwa niaba yake).
e) Atafariki dunia (mwanachama anapofariki dunia haki zake zote
zitahamishiwa kwa mrithi wake au kama aliweza kutoa maagizo yoyote
yatafuatwa).
f) Kupata ulemavu wa kudumu (kwa mwenye ulemavu wa kudumu hisa na
akiba zake zitaweza kurejeshwa kwa kulingana na aina ya ulemavu au
uamuzi wake mwenyewe).
Amana za mwanachama wa LAKWAO T SACCOS LTD zinaweza kuchukuliwa
wakati wowote ule kulingana na masharti ya chama. Mwanachama aliyepoteza
sifa za uanachama anaweza kuweka amana katika chama.
SEHEMU YA VII
USALAMA WA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA
Ili kuhakikisha kuwa fedha za wanachama na wateja wa LAKWAO T SACCOS LTD
zinakuwa salama mambo yafuatayo yatazingatiwa:-
a) Fedha zote zitapokelewa na mwenye mamalaka ya kupokea fedha kwa
niaba ya chama (mweka hazina)
b) Chama kitaajiri mweka hazina mwenye ujuzi na uaminifu wa hali ya juu
c) Ofisi ya chama italindwa na mlinzi mwenye silaha ya masafa ya mbali
d) Fedha zitawekewa bima
e) Fedha zitahifadhiwa katika benki ya CRDB isipokuwa kiwango/kiasi
kidogo kwa matumizi ya dharura.
f) Ofisi ya chama itakuwa kwenye jengo imara na la kudumu
g) Kutakuwa na kasiki kwa ajili ya kutunzia kiasi kidogo cha fedha
h) Kiasi cha fedha cha chini kabisa kitakachotunzwa katika kasiki kwa
matumizi ya dharura kitakuwa Tshs. 500,000/=
8
SEHEMU YA VIII
RIBA JUU YA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA
LAKWAO T SACCOS LTD inaweza kutoa riba/faida juu ya akiba na amana za
mwanachama. Riba inayoweza kutolewa kwa ajili ya akiba na amana
zilizowekwa na wanachama itakuwa pungufu kwa asilimia moja (1%) ya ile
(riba) inayotolewa na benki ya NMB/CRDB kwa mwaka.

MASHARTI LAKWAO(2008)TSACCOS LTD

1
Namba ya kuandikishwa . ……………………
MASHARTI
YA
CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO
CHA
LAKWAO TALANTA
SAVINGS AND CREDIT COOPERATIVE SOCIETY (2008) LTD.
LALTA
OVADA KWAMTORO
2
YALIYOMO
YALIYOMO ...................................................................................................................... 2
MASHARTI YA LAKWAO TSACCOS LTD ............................................................... 4
TAFSIRI YA VIFUPISHO AU MANENO .................................................................. 4
SEHEMU YA KWANZA ................................................................................................ 5
1.0 JINA NA ENEO LA SHUGHULI ................................................................... 5
2.0 OFISI NA ANUANI ......................................................................................... 5
SEHEMU YA PILI ............................................................................................................ 5
3.0 MADHUMUNI YA CHAMA- Kilimo na biashara .................................. 5
SEHEMU YA TATU ........................................................................................................ 6
4.0 UANACHAMA ................................................................................................. 6
4.1 AINA YA UANACHAMA .............................................................................. 6
4.2 MAKUNDI YA UANACHAMA .................................................................... 6
4.3 SIFA ZA UANACHAMA ................................................................................. 6
4.4 MAOMBI YA UANACHAMA....................................................................... 7
4.5 KUACHA NA KUSIMAMISHWA UANACHAMA .................................. 7
4.6 KUTEUA MRITHI ............................................................................................ 8
4.7 WAJIBU NA HAKI ZA MWANACHAMA ................................................ 8
5.7.1 WAJIBU WA MWANACHAMA .......................................................... 8
5.7.2 HAKI ZA MWANACHAMA .................................................................. 8
4.8 WAJIBU WA TSACCOS ................................................................................. 9
SEHEMU YA TANO ....................................................................................................... 9
5.0 KIINGILIO, HISA, AKIBA NA AMANA .................................................... 9
5.1 KIINGILIO ......................................................................................................... 9
5.2 HISA .................................................................................................................... 9
6.2.1 KUUZA AU KUHAMISHA HISA ........................................................ 10
5.3 AKIBA ............................................................................................................... 10
5.4 AMANA............................................................................................................ 10
SEHEMU YA SITA......................................................................................................... 10
6.0 MIKOPO KUTOKA TAASISI ZA FEDHA ................................................ 10
SEHEMU YA SABA ....................................................................................................... 11
7.0 VYANZO VYA MAPATO, HIFADHI NA UWEKEZAJI ....................... 11
7.1 VYANZO VYA MAPATO ............................................................................ 11
7.2 MTAJI WA TSACCOS ................................................................................... 11
7.3 HIFADHI NA UWEKEZAJI ......................................................................... 11
SEHEMU YA NANE ...................................................................................................... 11
8.0 UHASIBU NA MWAKA WA FEDHA ....................................................... 11
SEHEMU YA TISA..................................................................................................... 12
9.0 MGAO WA ZIADA ....................................................................................... 12
SEHEMU YA KUMI ...................................................................................................... 13
10.0 TARATIBU ZA UTUNZAJI WA AKIBA ............................................... 13
SEHEMU YA KUMI NA MOJA ................................................................................. 14
3
11.0 TARATIBU ZA MIKOPO ......................................................................... 14
SEHEMU YA KUMI NA MBILI ................................................................................. 15
12.0 UONGOZI NA USIMAMIZI .................................................................... 15
12.1 UONGOZI .................................................................................................... 15
13.2.1 UCHAGUZI WA VIONGOZI ........................................................... 15
12.2 USIMAMIZI ................................................................................................. 16
13.2.1 BODI YA TSACCOS ............................................................................ 16
13.2.2 KAMATI YA MIKOPO ...................................................................... 18
13.2.3 KAMATI YA USIMAMIZI ................................................................. 19
13.2.4 KAZI ZA MWENYEKITI WA TSACCOS ........................................ 20
13.2.5 KAZI ZA KATIBU / MENEJA WA TSACCOS .............................. 20
13.2.6 KAZI ZA MWEKA HAZINA ............................................................. 21
SEHEMU YA KUMI NA TATU .................................................................................. 22
13.0 MIKUTANO MIKUU ................................................................................ 22
13.1 Mkutano Mkuu wa Mwaka .................................................................... 22
13.2 MIKUTANO MIKUU YA KAWAIDA ................................................... 23
13.3 MKUTANO MKUU MAALUM ............................................................... 23
13.4 KUITISHA MIKUTANO MIKUU ........................................................... 23
13.5 AKIDI KATIKA MIKUTANO .................................................................. 24
SEHEMU YA KUMI NA NNE .................................................................................... 25
14.0 UIDHINISHAJI NA UWEKAJI SAINI KUMBUKUMBU ZA
TSACCOS .................................................................................................................... 25
SEHEMU YA KUMI NA TANO ................................................................................. 25
15.0 UKOMO WA MADENI ............................................................................ 25
SEHEMU YA KUMI NA SITA .................................................................................... 25
16.0 MUHURI WA TSACCOS “COMMON SEAL” ..................................... 25
SEHEMU YA KUMI NA SABA ................................................................................... 25
17.0 MAREKEBISHO YA MASHARTI ............................................................ 25
SEHEMU YA KUMI NA NANE ................................................................................. 25
18.0 KUVUNJWA AU KUFUTWA KWA TSACCOS .................................. 25
SEHEMU YA KUMI NA TISA .................................................................................... 26
19.0 MENGINEYO ............................................................................................... 26
4
MASHARTI YA LAKWAO TSACCOS LTD
(Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha LAKWAO Talanta. SACCOS
LTD)
Namba ya kuandikishwa ……………………… tarehe ya kuandikishwa
…………………………….
TAFSIRI YA VIFUPISHO AU MANENO
Kwa madhumuni ya masharti haya maneno haya yatatafsiriwa Kama ifuatavyo:-
TSACCOS: Talanta Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo
KIINGILIO: Fedha inayolipwa na mwanachama anapojiunga na chama na
hairudishwi.
HISA: Dhamana anayonunua mwanachama anayeomba kujiunga na
chama ili kuchangia mtaji wa chama.
AKIBA: Fedha ambazo mwanachama anaweka chamani mara kwa
mara ili kujenga fungu la kukopeshana.
AMANA: Fedha anayoweka mwanachama au asiye mwanachama kwa
ajili ya hifadhi. Amana inaweza kutumika kama kigezo na
dhamana ya mkopo.
KIKUNDI: Taasisi iliyoundwa na watu 10 – 15 (wakulima au
wafanyakazi au wafanyabiashara kwa makusudi ya kiuchumi
au kijamii).
MWANACHAMA: Ni mtu au taasisi iliyojiunga na chama na kukubali kufuata
masharti ya chama.
MRAJIS: Ni mtumishi wa umma aliye na mamlaka ya kuandikisha au
kufuta chama cha ushirika kwa mujibu wa sheria ya vyama
vya ushirika.
KUANDIKISHWA: Kuingizwa katika daftari la serikali baada ya chama kutimiza
taratibu/masharti yanayotakiwa.
CHAMA: Ni Talanta Chama cha Ushirika wa Akiba na Mkopo
kilichoandikishwa.
SCULT: Ni shirikisho la vyama vya ushirika wa Akiba na mikopo
Tanzania (Savings and Credit Cooperative League of
Tanzania)
JINSI: Ni maumbile ya kuwa mwanamke au mwanaume.
TAASISI: Ni vyama vya wanajamii kama vikundi, shule/vyuo,
makanisa, misikiti, CBO, NGO.
CBO (Asasi): Ni Community Based Organisation
NGO (Azise): Ni Asasi ya jamii (Asasi Zisizo za Serikali)
NON Government Organisation
5
SEHEMU YA KWANZA
1.0 JINA NA ENEO LA SHUGHULI
(i) Jina la chama litakuwa LAKWAO TSACCOS (LAKWAO Talanta
Savings and Credit Cooperative Society (2008) Ltd).
(ii) Eneo la shughuli la LAKWAO TSACCOS NI KATA za LALTA,
KWAMTORO na OVADA.
(iii) Mfungamano wa uanachama WAKULIMA, WAFUGAJI, WAFANYA
BIASHARA NA WAFANYAKAZI.
2.0 OFISI NA ANUANI
(i) LAKWAO T.SACCOSS Box 1187 DODOMA.
(ii) Makao Makuu OVADA.
SEHEMU YA PILI
3.0 MADHUMUNI YA CHAMA- Kilimo na biashara
Madhumuni ya LAKWAO TSACCOS ni kuwawezesha na kuwapa
wanachama fursa ya kujiwekea akiba na kutoa huduma za kibenki kwa
masharti nafuu kwa wanachama na wasio wanachama ili waweze kukidhi
mahitaji mbalimbali ya kiuchumi na kijamii na hatimaye kuinua hali ya
kiwango cha maisha.
LAKWAO TSACCOS itafanya kazi zifutazo ili kutimiza madhumuni yake:
(a) Kuendeleza uanachama wa mtu mmoja mmoja na kukuza uwezo wao
kiuchumi ili kuwawezesha kujiwekea akiba, kukopa kwa ajili ya
shughuli za kiuchumi na kurejesha kwa wakati kupitia vikundi vya
wanachama 10 – 15.
(b) Kupokea kiingilio, hisa, akiba na amana kutoka kwa wanachama na
kutoa mikopo kwa kuzingatia kiwango cha akiba na amana za
mwanachama.
(c) Kujenga tabia ya kujiwekea Akiba na Amana na kuepuka matumizi
yasiyo ya lazima miongoni mwa wanachama.
(d) Kuweka viwango vya riba juu ya Akiba, Amana na Mikopo kwa
wanachama vinavyokidhi gharama za uendeshaji wa LAKWAO
TSACCOS.
(e) Kupanga utaratibu unaofaa wa kutunza na kuweka kinga ya fedha ya
wanachama dhidi ya hasara/majanga.
(f) Kuunda mtaji wa kutosha kuendesha shughuli za LAKWAO TSACCOS.
(g) Kujenga na kuimarisha uwezo wa wanachama kuendesha na kusimamia
chama kwa njia ya elimu ya Ushirika na ushirikishwaji wa wanachama.
6
(h) Kubuni utaratibu mzuri wa kutosha taarifa za shughuli za LAKWAO
TSACCOS kwa wanachama na kupokea maombi ya Wanachama
wapya.
(i) Kununua hisa na dhamana (bond) kwenye vyombo vya fedha na
serikali baada ya kufanya utafiti wa kina wa kitaalamu.
(j) Kuwawezesha wanachama kuongeza kipato katika kaya na kusaidia
kuongezeka kwa mzunguko wa fedha katika eneo lao kwa kuhakikisha
kuwa huduma na mahitaji muhimu yanapatikana kwa urahisi katika
eneo la LAKWAO TSACCOS.
(k) Kutoa elimu ya ujasiriamali, uendeshaji na usimamizi wa biashara kwa
wanachama.
(l) Kushirikiana na taasisi nyingine za fedha na vyama vingine vya akiba na
mikopo kwa ajili ya kuongeza mtaji wa chama na kusaidiana.
(m) Kufanya shughuli nyingine muhimu kwa manufaa ya wanachama na
ustawi wa LAKWAO TSACCOS.
SEHEMU YA TATU
4.0 UANACHAMA
4.1 AINA YA UANACHAMA
Uanachama wa LAKWAO TSACCOS utakuwa na aina mbili kama
ifuatavyo:
(i) Uanachama wa HIARI kwa mtu mmoja mmoja ndani ya kikundi cha
wanachama 10 – 15 bila kujali jinsi.
(ii) Uanachama wa HIARI wa Taasisi kama vikundi, shule/vyuo, Vijiji,
makanisa, misikiti, CBO, NGOs.
4.2 MAKUNDI YA UANACHAMA
Uanachama utajumuisha makundi yafuatayo:-
(i) Wanachama waanzilishi wote waliohudhuria mkutano wa kwanza
na ambao wametimiza masharti haya.
(ii) Wanachama watarajiwa ambao watajiunga kwa kuomba na
kujadiliwa na bodi ya chama.
4.3 SIFA ZA UANACHAMA
(a) Awe mwenye umri wa miaka isiyopungua 18
(b) Awe na akili timamu.
(c) Awe mwaminifu na mwadilifu
(d) Awe raia wa Tanzania mkaazi wa eneo la shughuli za LAKWAO
TSACCOS.
(e) Awe amelipa kiingilio na angalu hisa moja
(f) Asiwe ni mtu mwenye kufanya shughuli zinazoshabihiana na LAKWAO
TSACCOS.
7
(g) Awe tayari kufuata masharti ya LAKWAO TSACCOS, kanuni za vyama
vya ushirika ya 2004 na sheria ya vyama vya ushirika Na. 20 ya mwaka
2003.
4.4 MAOMBI YA UANACHAMA
Maombi ya uanachama kwa kikundi au mtu mmoja mmoja yatafanywa
kwa kujaza fomu maalum. Maombi ya mtu mmoja mmoja yatafanywa
kwa kupitia kwenye kikundi chake na hatimaye kwenda kwenye Bodi ya
uongozi ya LAKWAO TSACCOS, ambapo mwenye kutimiza sifa
atapokelewa na kulipa michango yote kwa mujibu wa masharti haya.
Mwanachama atakayepokelewa ataorodheshwa kwenye daftari la
wanachama. Watakaokataliwa watajulishwa kwa maandishi. Maombi
yote ya wanachama wapya yatathibitishwa na mkutano mkuu.
4.5 KUACHA NA KUSIMAMISHWA UANACHAMA
(a) Mwanachama anaweza kuacha uanachama kwa kutoa taarifa ya
maandishi.
(b) Mwanachama anaweza kusimamishwa uanachama na Bodi ya Uongozi
endapo:-
(i) Atashindwa kulipa mkopo wake katika muda ulioruhusiwa na
LAKWAO TSACCOS, kukosa uaminifu na uadilifu au kufanya
kitendo ambacho ni kinyume na madhumuni ya LAKWAO
TSACCOS.
(ii) Kuacha kushiriki shughuli za TSACOSS (kushindwa kuweka Akiba
na Amana kwa mwaka mmoja).
Kusimamishwa kutahesabika tangu tarehe ya kutoa uamuzi wa
kusimamishwa mwanachama.
(c) Uanachama utakoma kwa:-
(i) Kifo
(ii) Kuchukua hisa zake zote kwenye LAKWAO TSACCOS
(iii) Kujiuzulu mwenyewe baada ya kutoa taarifa ya miezi mitatu
(siku 90) kwa maandishi kwa TSACCOS kwa kipindi yawe
yamekamilika na kukubalika na Mkutano Mkuu.
(iv) Ugonjwa wa akili uliothibitishwa na Daktari.
(v) KUhama katika eneo la shughuli za LAKWAO TSACCOS.
(vi) Kufukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu kwa kura ya
wanachama wasiopungua nusu ya wanachama waliohudhuria,
baada ya kupewa nafasi ya kujitetea kutokana na makosa
ambayo yanasababisha kufukuzwa.
8
4.6 KUTEUA MRITHI
Kila mwanachama atateua mrithi wake ambaye atakuwa na haki ya
kulipwa hisa, akiba, amana na fidia zote za LAKWAO TSACCOS baada ya
makato yote ya madeni anayodaiwa na chama. Mwanachama ana haki ya
kubadilisha jina la mrithi. Kila uteuzi utaandikwa katika daftari ya
wanachama na mwanachama anayehusika atatia saini. Pia mrithi anaweza
kurithi hisa, akiba, amana, faida na madeni.
4.7 WAJIBU NA HAKI ZA MWANACHAMA
Mwanachama yeyote atakuwa na wajibu na haki kama ifuatavyo:-
5.7.1 WAJIBU WA MWANACHAMA
i) Kulipa kiingilio, kununua hisa na kuweka Akiba na Amana na
masharti ya LAKWAO TSACCOS hii.
ii) Kulipa mkopo muda uliopangwa kulingana na masharti ya
LAKWAO TSACCOS.
iii) Kulipa mkopo alioudhamini endapo mkopaji atashindwa
kulipa mkopo wake.
iv) Kuwa mwaminifu kwa LAKWAO TSACCOS na kushiriki
kikamilifu katika shughuli zote ili kuiwezesha LAKWAO
TSACCOS kutimiza madhumuni yake.
v) Kubeba dhamana endapo janga lolote litatokea.
vi) Kuweka akiba mara kwa mara
vii) Kukopa kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali (kiuchumi)
viii) Kuhudhuria na kushiriki kikamilifu katika mikutano.
5.7.2 HAKI ZA MWANACHAMA
i) Kushiriki katika shughuli zote za TSACCOS hii kwa kufuata
sheria ya ushirika namba 20 ya mwaka 2003, kanuni za
vyama vya ushirika za mwaka 2004, masharti ya LAKWAO
TSACCOS na maazimio yote ya Mkutano Mkuu wa
wanachama.
ii) Kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya
TSACCOS.
iii) Kuchagua na kuchaguliwa kuwa mjumbe/kiongozi.
iv) Kuweka na kuchukua akiba, amana na zake kwa kufuata
masharti ya LAKWAO TSACCOS hii.
v) Kuwa mdhamini wa mikopo kwa mwanachama mwingine
ndani ya kikundi chake.
vi) Kupatiwa taarifa ya maendeleo ya LAKWAO TSACCOS.
Kuwa masharti, kutazama mizania, mihtasari ya Mikutano
Mikuu na nyaraka za Mrajis wakati wa saa za kazi.
vii) Kuomba kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu wa kifungu
15.35 cha masharti haya.
viii) Kupatiwa mkopo kwa ajili ya kuongeza tija na maendeleo ya
kiuchumi.
9
ix) Mwanachama atakuwa na wajibu kama ilivyo kwenye
kifungu cha 40, 41 na 42 cha Sheria ya Vyama vya Ushirika
ya mwaka 2003.
x) Katika kufilisika chama, mwanachama atawajibika kwa
kiwango cha hisa ambacho analazimika kulipa.
4.8 WAJIBU WA TSACCOS
i) Kutowabagua wanachama
ii) Kuweka mazingira bora kwa mwanachama ya kuweka akiba, amana
na kukopa.
iii) Kutunga masharti ya sera bayana kwa mwanachama.
iv) Kulinda maslahi ya wanachama.
v) Kuhamasisha wanachama watarajiwa hususan wanawake kujiunga
na LAKWAO TSACCOS
SEHEMU YA TANO
5.0 KIINGILIO, HISA, AKIBA NA AMANA
Kiwango cha kiingilio, Hisa, Akiba na Amana kitakuwa kinapangwa na
Mkutano Mkuu kila inapobidi kulingana na thamani ya fedha.
5.1 KIINGILIO
Mwanachama lazima alipe kiingilio katika kipindi cha kukubalika kwake
uanachama. Kiingilio hakirejeshwi Kwa mwanachama akiacha uanachama
au kusimamishwa uanachama na wala hakizai faida. Kiwango cha kiingilio
kitapangwa kila mara na Mkutano Mkuu. Kiingilio kitakuwa 5,000/=
fedha za kitanzania.
5.2 HISA
(a) Thamani ya hisa moja ni shilingi 5,000/= fedha za kitanzania.
(b) Mwanachama inabidi anunue hisa nyingi kwa faida yake mwenyewe na
ya TSACCOS yake lakini isizidi 1/5 ya hisa zote za TSACCOS.
(c) Mwanachama anaweza kununua hisa moja au zaidi kwa wakati mmoja
na kuingizwa kwenye daftari la orodha ya wanachama.
(d) Mwanachama atakayekamilisha ununuzi wa hisa zote atapewa hati ya
hisa.
(e) Ili uwe mwanachama, mwanachama anatakiwa awe amenunua si chini
ya hisa 1 na kuwa ametimiza kununua hisa angalau 2 katika kipindi cha
mwaka mmoja na hisa angalau 10 zinunuliwe katika kipindi cha mwaka
wa pili.
(f) Mwanachama akiachishwa uanachama atarudishiwa hisa na akiba
pamoja na amana zake zote katika kipindi cha siku 90 iwapo hadaiwi
na LAKWAO TSACCOS.
10
6.2.1 KUUZA AU KUHAMISHA HISA
a) Hisa zinaweza kurithiwa, kuuzwa au kuhamishwa.
b) Mwanachama wa LAKWAO TSACCOS anaweza kununua hisa za
mwanachama ambaye uanachama wake umekoma.
c) Mwanachama akishindwa kukamilisha hisa zake zote katika kipindi cha
miaka miwili, hisa alizonunua zitahesabiwa kuwa zimefutika.
5.3 AKIBA
a) Kila mwanachama lazima ajenge tabia ya kuweka akiba mara kwa mara
kwa ajili ya kujenga fungu la kukopeshana.
b) Kila mwanachama ataweka si chini ya asilimia 10 ya mapato yake
anayoyapata kwa vipindi tofauti.
c) Akiba za mwanachama zitachukuliwa kama dhamana na kigezo cha
kupata mkopo kulingana na sera ya mikopo, akiba na amana, na
zitakuwa hazitolewi au kupunguzwa mara kwa mara.
d) Mwanachama mpya anapaswa kuweka akiba yake mfululizo zaidi ya
miezi sita bila kupata mkopo isipokuwa pale ambapo LAKWAO
TSACCOS itakuwa na fedha za kutosha kukopesha wanachama wapya.
e) Kuweka akiba ni lazima katika TSACCOS.
5.4 AMANA
a) Mwanachama anaweza kuweka amana katika LAKWAO TSACCOS.
b) Wasio wanachama nao wanaweza kuweka amana kwa ajili ya kupata
huduma za kibenki kwa kulipia gharama zitakazoamuriwa na LAKWAO
TSACCOS.
c) Amana zinaweza kuchukuliwa muda wowote ule ambapo aliyeweka
anahitaji kuchukua
d) Fedha za amana zinaweza kutumika katika kukopesha wanachama na
kama dhamana ya mkopo kwa mkopaji.
SEHEMU YA SITA
6.0 MIKOPO KUTOKA TAASISI ZA FEDHA
a) LAKWAO TSACCOS inaweza kukopa baada ya kupata idhini ya
Mkutano Mkuu na Mrajis wa vyama Ushirika.
b) LAKWAO TSACCOS inaweza kukopa kiasi kisichozidi robo (1/4) ya
jumla ya hisa zote pamoja na akiba, amana kwa uamuzi wa angalau
robo (3/4) ya wajumbe wa Bodi ya Uongozi.
c) Kiasi zaidi kinaweza kukopwa baada ya kupata uamuzi wa wanachma
kwenye Mkutano Mkuu ambao wataafiki pendekezo lililofanywa na
robo tatu (3/4) ya wajumbe wa Bodi ya Uongozi. Lakini kiasi
kitakachokopwa kisizidi nusu ya raslimali ya TSACCOS.
11
d) Dhamana ya mwanachama kwa ajili ya madeni ya TSACCOS haitazidi
kiwango cha hisa zake ndani ya TSACCOS ziwe zimelipwa au bado.
SEHEMU YA SABA
7.0 VYANZO VYA MAPATO, HIFADHI NA UWEKEZAJI
7.1 VYANZO VYA MAPATO
Mapato ya TSACCOS yatatokana na:-
a) Viingilio
b) Hisa za wanachama
c) Akiba za wanachama
d) Amana za wanachama na wasio wanachama
e) Michango maalum, ruzuku na misaada
f) Akiba na malimbikizo ya lazima
g) Faida zitokanazo na shughuli za chama
h) Mikopo kutoka mabenki na taasisi nyingine za fedha
i) Mapato yatokanayo na vyanzo vinginevyo
7.2 MTAJI WA TSACCOS
Mtaji wa LAKWAO TSACCOS utatokana na:-
a) Hisa za wanachama
b) Ziada halisi
c) Akiba ya lazima na malimbikizo
d) Michango maalum, ruzuku na misaada
Mapato ya LAKWAO TSACCOS yatatumika kwa shughuli za maendeleo ya
LAKWAO TSACCOS ili kuweza kufikia madhumuni yake kwa idhini ya
Mkutano Mkuu wa wanachama.
7.3 HIFADHI NA UWEKEZAJI
LAKWAO TSACCOS itahifadhi na kuwekeza fedha kama ifuatavyo:-
a) Kwa kutumia mtaji wake kununua amana za serikali.
b) Kutoa mikopo kwa wanachama
c) Kununua hisa kwenye vyombo vya fedha na makampuni n.k.
d) Kujenga nyumba na kununua mali isiyohamishika
e) Fedha zote za LAKWAO TSACCOS lazima ziwekewe bima.
f) Fedha za LAKWAO TSACCOS isipokuwa zile zinazohitajika kwa
matumizi madogo madogo zitahifadhiwa benki. Bodi itaamua kiasi cha
fedha kitakachobaki kwa matumizi madogo madogo na kwa ajili ya
kulipia amana.
SEHEMU YA NANE
8.0 UHASIBU NA MWAKA WA FEDHA
12
(a) Mwaka wa fedha wa chama utakuwa kuanzia tarehe 1 Julai hadi tarehe
31 Juni.
(b) LAWAO TSACCOS itaandika vitabu vya hesabu na kutunza
kumbukumbu muhimu kwa kuzingatia mfumo ulioidhinishwa na Mrajis
wa vyama vya ushirika na kanuni za uhasibu.
(c) Hesabu za TSACCOS zitaandikwa kila siku.
(d) Kamati ya Usimamizi ya LAKWAO TSACCOS itapitia mfumo wa hesabu
na utunzaji kumbukumbu za TSACCOS kila mwaka kwa kushirikiana na
mkaguzi wa LAKWAO TSACCOS. Wajumbe wa Kamati wanaweza
kuchunguza vitabu na kumbukumbu za TSACCOS wakati wowote wao
wenyewe au kwa kushirikiana na Maafisa Ushirika.
(e) Vitabu vya LAKWAO TSACCOS vitakaguliwa na mizania kutolewa
kulingana na Sheria ya Vyama Ushirika Na. 20 ya mwaka 2003, na
mkaguzi yeyote atakayechaguliwa na chama.
(f) Gharama za ukaguzi zitalipwa na LAKWAO TSACCOS yenyewe.
(g) TSACCOS itakuwa na “Mfumo wa Uhasibu” na “Kanuni za Fedha”.
(h) LAKWAO TSACCOS itatengeneza makisio ya mapato na matumizi na
kupitishwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirka mwezi mmoja kabla ya
kuanza mwaka mpya wa biashara.
SEHEMU YA TISA
9.0 MGAO WA ZIADA
Bodi ya Uongozi ya LAKWAO TSACCOS itatoa mapendekezo ya mgao wa
ziada ya mwaka na miaka iliyopita baada ya ukaguzi wa mahesabu na
mizania kutolewa; kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama ili uidhinishwe
kwa kuzingatia kifungu cha 67 cha kanuni za vyama vya ushirika za 2004.
(a) Kiasi kisichopungua asilimia (20%) kitatengwa kutokana na faida halisi
kwa ajili ya akiba ya lazima. Akiba ya lazima itabakia kuwa ni mali ya
TSACCOS na haitawezekana kugawanywa isipokuwa kama
kinavunjwa. Viingilio vyote, adhabu mbalimbali na gharama za
uhamisho wa Hisa zitaongezwa katika akiba hii baada ya kutoa
gharama za kuandikishwa TSACCOS.
(b) Asilimia kumi na tano (15%) kwa ajili ya mfuko wa kukombolea hisa za
walioacha uanachama isipokuwa kiasi hicho kisizidi asilimia kumi na
tano (15%) ya hisa zote.
(c) Asilimia kumi na tano (15%) ya faida halisi itatengwa kwa ajili ya kinga
ya madeni mabaya. Isipokuwa kiasi hicho kisizidi asilimia kumi na tano
(15%) ya madeni yote.
(d) Ziada inayobaki itagawanywa kama itakavyoamuliwa na Mkutano
Mkuu kwa ajili ya:-
13
(i) Mgao wa ziada kwa wanachama au faida ya hisa;
(ii) Nyongeza za hisa wanachama;
(iii) Mchango kwa shughuli za maendeleo ya LAKWAO TSACCOS.
(iv) Mchango au msaada kwa ajili ya elimu, afya, au shughuli
nyingine yeyote.
(e) Tuzo kwa wajumbe wa bodi ya uongozi na watumishi wasiolipwa
mishahara.
(f) Malipo mengine yoyote kama yatakavyoamuliwa ikiwa ni pamoja na
kubakiza kwa mwaka unaofuata.
SEHEMU YA KUMI
10.0 TARATIBU ZA UTUNZAJI WA AKIBA
Akiba za mwanachama zitatunzwa kwa kufuata taratibu zifuatazo:-
a) Kila mwanachama atapatiwa kitabu cha akiba (pass – Book)
b) Kitabu cha akiba kitaonyesha jina mwanachama, namba ya kitabu na
uanachama
c) Katika kitabu cha mwanachama zitaingizwa hesabu za Hisa, Akiba,
Amana na Mikopo
d) Kutakuwa na daftari la kutolea vitabu vya akiba vya wanachama.
e) Fedha yote ya mwanachama inayopokelewa ndani ya TSACCOS
ikatiwe stakabadhi ya fedha na kuingizwa katika kitabu chake (Pass
Book) na kutiwa saini na Mweka Hazina au mtu mwingine
aliyeidhinishwa kupokea fedha, kisha kitabu hicho atapewa
mwanachama mwenyewe akitunze.
f) Ikiwa kitabu kitapotea mwanachama anayehusika atawajibika kutoa
taarifa ya maandishi kwa Mweka Hazina/Katibu. Bodi inaweza
kuidhinisha kitabu kingine kitolewe na mwenye kitabu atalipa ada ya
kitabu kipya kadri itakavyoamuliwa na bodi. Kitabu kipya kitaingizwa
salio za hesabu zote za mwanachama kama zilivyo kwa tarehe
anayopatiwa kitabu kipya kutoka kwenye leja ya mwanachama.
g) Kitabu cha akiba hakina budi kionyeshwe wakati wote wa kuweka
fedha au wakati wa kuchukua fedha ili Mweka Hazina aweze kuingiza
kiasi kilichowekwa au kuchukuliwa na mwanachama.
14
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
11.0 TARATIBU ZA MIKOPO
(a) Mikopo itatolewa kwa wanachama wa LAKWAO TSACCOS tu.
(b) Maombi yote ya Mikopo yataidhinishwa na kamati ya mikopo,
ambayo lazima ihakikishe kuwa taratibu na masharti ya utoaji mikopo
yamezingatiwa na mkopaji.
(i) Mikopo ya dharura italipwa katika kipindi kisichozidi miezi 3 na
kwa kadri itakavyoamuliwa na kamati ya mikopo.
(ii) Mikopo ya maendeleo italipwa katika kipindi kisichozidi miezi
36 na kwa kadri itakavyoamuliwa na kamati ya mikopo.
(c) Fomu maalum ya maombi ya mkopo lazima ijazwe na kila mwombaji
na kuwasilisha kwa mhusika. Mwombaji atoe taarifa sahihi za uwezo
wa kulipa mikopo mingine aliyonayo.
Kamati ya mikopo itapitia maombi ya mkopo ikizingatia dhamana ya
mkopo kama inatosha, uwezo wa kulipa mikopo ya
LAKWAOTSACCOS.
(d) Mwombaji lazima awe na akiba na amana na adhaminiwe na
mwanachama mwenzake/kikundi chake. Mwanachama haruhusiwi
kudhamini zaidi ya mikopo miwili.
(e) Kwa wajumbe wa bodiyauongozi, kamati ya mikopo au kamati ya
usimamizi, mikopo yao itapaswa kudhaminiwa na wanachama wengine
kama mwanachma mwingine yeyote.
(f) Miradi inayopatiwa mikopo itakuwa pia dhamana ya mikopo hiyo
mpaka mlipaji atakaporejesha mikopo na salio kuwa sawa na kiasi cha
hisa au akiba alizonazo ndani ya TSACCOS.
(g) Urejeshaji wa mikopo utafanywa kwa kulipa fedha taslimu, hundi au
kukatwa kwenye mshahara au vyote kwa pamoja katika ofisi ya
TSACCOS wakati wa saa za kazi, au muda mwingine utakaopangwa.
(h) Baada ya mkopo kuidhinishwa mkopaji atajaza fomu maalum ya
mkataba ambayo itatiwa saini na wadhamini. Fomu hii itaonyesha
masharti ya mkopo.
(i) Maombi ya mwanakamati wa mikopo yatajadiliwa na wanakamati
waliobaki ili mradi akidi inatosha.
(j) Iwapo TSACCOS imepata mkopo toka sehemu nyingine itakopesha
kulingana na masharti ya mkopo huo (mfano faida au jinsi).
15
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
12.0 UONGOZI NA USIMAMIZI
12.1 UONGOZI
(a) TSACCOS itaongozwa na Bodi ya Uongozi ambayo itaundwa na
wajumbe wasiopungua watano na wasiozidi tisa ikiwa ni pamoja na
Mwenyekiti na Makamu wake.
(b) Wajumbe wa Bodi watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa TSACCOS
na muda wao wa ofisi utakuwa miaka mitatu lakini wanaweza
kuchaguliwa tena na kila baada ya miaka mitatu 1/3 ya wajumbe wa
Bodi watajiuzulu. Wale waliojiuzulu hawapaswi kuchaguliwa tena
mpaka baada ya miaka mitatu.
(c) Kutakuwa na Kamati ya mikopo ambayo itachaguliwa na wanachama
kutoka miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya uongozi. Kamati hii
itakuwa na wajumbe watatu. Kamati hii inaweza ikachaguliwa pia na
wanachama kutoka nje ya wajumbe wa Bodi ya uongozi.
(d) Kutakuwa na Kamati ya usimamizi ya wajumbe watatu ambayo
itachaguliwa na Mkutano Mkuu wa wanachama kutoka miongoni
mwao.
(e) Bodi ya Uongozi inaweza kuunda kamati zingine ndogo kama vile
kamati ya elimu na uhamasishaji na kuteua wajumbe kulingana na
mahitaji.
13.2.1 UCHAGUZI WA VIONGOZI
Uchaguzi wa Bodi ya Uongozi utafanyika kwa mujibu wa kifungu cha 63
cha Sheria ya vyama vya ushirika Na. 20 ya mwaka 2003 pamoja na
Kanuni ya 42 na 43 ya vyama vya ushirika ya 2004.
Hatua zifuatazo zitafuatwa wakati wa uchaguzi wa Bodi ya Uongozi:-
(a) Kila mwanachma anayetaka kugombea nafasi ya ujumbe wa bodi
atajaza fomu maalum zilizoandaliwa na kuzirudhisha kwa msimamizi
wa uchaguzi ndani ya tarehe itakayokuwa imeelekezwa.
(b) Kamati ya uchaguzi itafanya mchujo wa wagombea kwa kuweka alama
walizopata kutokana na maelezo binafsi na uzoefu wao. Watakaopata
chini ya alama 40 hawapendekezwi.
16
(c) Inapofika agenda ya uchaguzi wa viongozi, Mrajis Msaidizi/Afisa
Ushirika wa eneo la TSACCOS atasimamia uchaguzi na Mwenyekiti
atakayeongoza uchaguzi, Mwenyekiti huyo sharti atokane na miongoni
mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu.
(d) Wanachama wapendekeze idadi ya wajumbe wa bodi wanaohitajika
kulingana na maendeleo ya chama.
(e) Majina ya wagombea waliopendekezwa na kamati ya uchaguzi
yatasomwa na msimamizi wa uchaguzi.
(f) Uchaguzi wa wajumbe wa bodi utafanywa kwa kupigiwa kura ya siri
tu na wala siyo vinginevyo.
(g) Mara tu baada ya uchaguzi, kura zitahesabiwa na matokeo
kutangazwa na Mwenyekiti wa Mkutano.
(h) Uchaguzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Mtunza
hazina utafanywa moja kwa moja na Mkutano Mkuu.
(i) Uchaguzi wa Kamati ya Mikopo, Kamati ya usimamizi na kamati
ndogo ya Elimu na uhamasishaji utafanywa na Mkutano Mkuu.
(j) Nafasi ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti iwapo itagombewa na
mtu mmoja bila upinzani kura za siri sio lazima zipigwe.
12.2 USIMAMIZI
13.2.1 BODI YA TSACCOS
(a) Bodi ya TSACCOS itachaguliwa na Mkutano Mkuu wa wanachama
wote.
(b) Bodi ya TSACCOS itafanya Mkutano angalau mmoja kila baada ya
miezi mitatu.
(c) Bodi itapokea na kujadili taarifa za maendeleo ya TSACCOS kutoka
kwa kamati na watendaji wa chama.
(d) Bodi ya TSACCOS itateua mwanachama atakayeshika nafasi iliyoachwa
wazi katika Bodi hiyo na Kamati za usimamizi na mikopo.
Watkaoteuliwa watashika nafasi hizo mpaka mkutano mkuu mwingine
unaofuata ambapo nafasi zilizowazi zitajazwa kwa kura za wanachama.
(e) Katibu wa vikao vya Bodi atakuwa Meneja wa TSACCOS au Katibu wa
kuchaguliwa kama TSACCOS itakavyoamua.
17
(f) Hakuna mjumbe atakayekuwa na haki ya kudai malipo ya mshahara au
posho isipokuwa kama ilivyoelezwa katika masharti haya.
(g) Mjumbe wa Bodi ataacha madaraka kama akifukuzwa na Mkutano
Mkuu/Kamati ya usimamizi au sababu yoyote kama ilivyo katika kanuni
za vyama vya ushirika za mwaka 2004 kifungu cha 42 (1).
(h) Mjumbe wa Bodi atakayeshindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo
bila sababu inayokubaliwa na kamati anaweza kuachishwa uongozi na
kuteua mwanachama mwingine badala yake hadi Mkutano Mkuu
unaofuata.
(i) Bodi itakuwa na mamlaka ya kusimamia shughuli zote za TSACCOS,
mbali na majukumu mengine bodi itakuwa na wajibu wa kufanya
mambo yafuatayo:-
(i) Kueneza elimu ya uwekaji akiba na utoaji mikopo kwa
kuwaelimisha wanachama kuhusu matumizi bora ya mikopo
yao.
(ii) Kupokea na kufikiria maombi ya wanachama wapya na
kuyafikisha mbele ya Mkutano Mkuu unaofuata kwa uthibitisho.
(iii) Kuhakikisha kuwa wakopaji wanalipa madeni yao kama
walivyoahidi na kuwachukulia hatua za kisheria wakopaji wasio
waaminifu, na kupendekeza kwa Mkutano Mkuu ufutaji wa
mikopo mibaya ambayo haiwezi kulipwa kabisa.
(iv) Kuweka utaratibu wa uendeshaji a shughuli za akiba na mikopo
ila kwa masharti kwamba taratibu hizo zisikiuke sheria na kanuni
za vyama vya ushirika za 2004, masharti na maagizo ya Mrajis
ya vyama vya ushirika.
(v) Kusimamia matumizi yote ya TSACCOS isipokuwa kazi za
kuidhinisha maombi ya mikopo kulingana na masharti ya utoaji
mikopo yaliyowekwa na TSACCOS na Mrajis wa vyama vya
ushirika.
(vi) Kuajiri, kusimamisha au kufukuza watumishi kazi kwa kuzingatia
sheria za ajira za TSACCOS (kanuni za utumishi).
(vii) Kufikisha mbele ya Mkutano Mkuu wa mwaka, mapendekezo ya
makisio, hesabu ya mapato na matumizi, mizani na taarifa ya
ukaguzi.
18
(viii) Kuandika na kutunza mihtasari ya Mikutano Mikuu na vikao vya
bodi katika kitabu cha kumbukumbu a mikutano na kutiwa saini
na Mwenyekiti na Katibu.
(ix) Kuendesha shughuli za TSACCOS katika misingi ya kibiashara.
Hasara yoyote itakayotokea katika TSACCOS kutokana na bodi
kutojali wajibu wao na madaraka waliyopewa na wanachama,
itawalazimu kufidia hasara hiyo kama itakavyoamuliwa na Mrajis
wa Vyama vya Ushirika, kwa mujibu wa sheria ya ushirika Na.
20 ya mwaka 2003 kifungu cha 93(1).
(x) Kusimamisha uanachama mwanachma au mjumbe yeyote wa
kamati ya mikopo au ya usimamizi kutokana na tabia mbaya au
kushindwa kutimiza wajibu wake wa kazi na kupeleka
mapendekezo katika Mkutano Mkuu unaofuata ili uamuzi wa
mwisho utolewe.
13.2.2 KAMATI YA MIKOPO
(a) Kutakuwa na kamati ya mikopo itakayokuwa na wajumbe watatu
ambao watachaguliwa na Mkutano Mkuu.
(b) Wajumbe wa kamati hii watashika madaraka yao kwa muda wa
miaka mitatu. Theluthi moja (1/3) ya wajumbe itajiuzulu kila baada
ya miaka mitatu na wanaweza kuchaguliwa tena kwa mujibu wa
kifungu 63 cha sheria ya ushirika Na. 20 ya mwaka 2003 na kanuni
za vyama vya ushirika za 2004 kifungu cha 39.
(c) Wajumbe wa kamati hii watachagua miongoni mwao, mwenyekiti na
Katibu. Kumbukumbu za mambo yote yatakayofanywa na kamati ni
lazima nakala ziwe tayari kwa muda usiozidi siku tatu, tangu shughuli
hizo zitendeke.
(d) Maombi yote ya mikopo yatafikiriwa na Kamati hii. Itahakikisha
kuwa mkopo unaoombwa ni wa manufaa kwa mkopaji. Itachuguza
dhamana iliyotolewa kama ni sawa.
(e) Kamati hii itawajibika kufuatilia matumizi bora ya mikopo na
kuhakikisha kwamba wakopaji wanatumia fedha kwa miradi au
shughuli waliyoombea mikopo hiyo.
(f) Kamati itafanya kikao angalau kimoja kila mwezi, lakini inaweza
kufanya kikao cha dharura wakati wowote. Hakuna mkopo
utakaotolewa pasipo kukubaliwa kwanza na wanakamati wote
ambao wamehudhuria katika kikao isipokuwa Kwa mikopo ambayo
19
Afisa wa mikopo amepewa kibali. Taarifa za mikopo zitatolewa Kwa
wanachama katika mikutano yao mikuu.
(g) Kamati ya mikopo itachunguza kwa uangalifu tabia na hali ya fedha
ya kila mwombaji wa mkopo pamoja na dhamana, kama zipo na,
kuhakikisha uwezo wa kulipa deni kwa ukamilifu katika muda
ulioweka.
(h) Kwa wingi wa kura, kamati ya mikopo inaweza kumchagua Afisa au
Maofisa wa mikopo, kufanya kazi kama itakavyohitajika na kamati na
kumpa uwezo wa kuidhinisha mikopo kwa kadri ya kiasi
kinachowekwa na kamati. Hataweza kuchaguliwa zaidi ya afisa
mmoja wa mikopo kutoka kwenye kamati. Kila afisa mikopo atatoa
kwa kamati kumbukumbu ya kila mkopo aliouidhinisha au alioukataa
kwa muda usiozidi siku saba tangu siku ya maombi yaliyopokelewa.
Mikopo yote isiyoidhinishwa na afisa mikopo, itashughulikiwa na
kamati ya mikopo. Hakuna mtu yeyote atakayekuwa na mamlaka ya
kulipa kutoka mfuko wa chama hiki, mkopo usioidhinishwa na
kamati ya mikopo au afisa mikopo (mhasibu au meneja wa TSACCOS
atakuwa afisa wa mikopo).
13.2.3 KAMATI YA USIMAMIZI
(a) Kutakuwa na kamati ya usimamizi ambayo itakuwa na wajumbe
watatu watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wenye maadili mema,
wapenda haki, wanaweza kusimamia kazi na kuchukua hatua za
kurekebisha dosari pasipo upendeleo.
(b) Wajumbe wa kamati hii watashika madaraka kwa muda wa miaka
mitatu na theluthi (1/3 ya wajumbe itajiuzulu kila baada ya miaka
miatatu na wanaweza kuchaguliwa tena kwa mujibu wa sheria ya
ushirika ya mwaka 2003).
(c) Wajumbe wa Kamati hii watatengeneza utaratibu wa kutekeleza kazi
zao. Watachagua Mwenyekiti na Katibu miongoni mwao. Katibu
atatengeneza na kuhifadhi kumbukumbu zote pamoja na hatua
zinazochukuliwa na kamati hii.
(d) Kamati itafanya kazi zifuatazo:-
(i) Kusimamia fedha na mali zote za TSACCOS kwa niaba ya
wanachama.
(ii) Kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za TSACCOS na
kuhakikisha kuwa zinazofanywa ipasavyo.
(iii) Kamati hi itatoa au itaamua ufanyike japo mara moja katika
miezi mitatu uchunguzi wa shughuli za TSACCOS pamoja na
20
ukaguzi wa vitabu. Kamati itatengeneza au itaamuru
utengenezaji wa taarifa itakayotolewa kwa Mkutano Mkuu
kwa maandishi na itakagua au itaamuru ukaguzi wa mwaka
ufanyike na taarifa yake itolewe kwa maandishi katika
Mkutano Mkuu wa mwaka ufuatao.
(iv) Kamati itafuatilia maendeleo ya miradi mikubwa ambayo
imepatiwa mkopo wa TSACCOS mpaka wahusika
watakapomaliza marejesho.
(v) Kutayarisha taarifa ya maandishi juu ya hali ya fedha na
huduma zitolewazo kwa Bodi na Mkutano Mkuu na nakala
kwa Afisa Ushirika wa Wilaya, Mkoa na SCCULT, kila miezi
mitatu ya mwaka wa fedha wa TSACCOS.
(vi) Kusikiliza malalamiko ya wanachama na kuyatafutia
ufumbuzi.
13.2.4 KAZI ZA MWENYEKITI WA TSACCOS
(a) Kusimamia / kuongoza mikutano yote mikuu isipokuwa Mkutano
Mkuu maalum uliotishwa na Mrajis.
(b) Kusimamia / kuongoza mikutano yote ya bodi ya uongozi
(c) Kuweka saini kumbukumbu za mikutano mikuu vikao vya bodi ya
uongozi
(d) Kuitisha mikutano yote mikuu na vikao vya bodi kufuatana na
masharti haya.
(e) Kuweka saini kwa niaba ya chama kumbukumbu zote na za mikataba
zinazohitaji kupigiwa muhuri wa chama.
(f) Kuwa msemaji mkuu wa chama kama haitaamuliwa vinginevyo na
bodi ya uongozi wa LAKWAO TSACCOS.
13.2.5 KAZI ZA KATIBU / MENEJA WA TSACCOS
Kazi, wajibu na madaraka ya Katibu / Meneja wa TSACCOS yatakuwa
kama ifuatavyo:-
(a) Kupokea barua zote na kuziwasilisha kwa wahusika kwa utekelezaji.
(b) Kujibu na kupeleka barua zote zitakiwazo baada ya maelezo ya
wahusika.
(c) Kuandaa Mikutano Mikuu na vikao vya LAKWAO TSACCOS.
(d) Kuweka mahali pa usalama fedha, vitabu, kumbukumbu na mali za
TSACCOS
(e) Kufanya mawasiliano yote kwa niaba ya LAKWAO TSACCOS
(f) Kutengeneza / kuandaa mipango ya maendeleo ya muda mrefu na
mfupi pamoja na makisio ya mapato na matumizi.
21
(g) Kushauri bodi ya uongozi kuhusu upatikanaji, uajiri, matumizi na
endeshaji watumishi
(h) Kushauri bodi ya uongozi katika shughuli za kifedha, kibiashara,
kiutaalamu na kiuongozi.
(i) Kusimamia na kuratibu mipango yote ya uchumi ya chama.
(j) Kutayarisha na kutengeneza taarifa za mwezi, robo, nusu na mwaka
mzima.
(k) Kuwa Katibu wa vikao vya bodi ya uongozi na Mikutano Mikuu na
kuandika kumbukumbu za mikutano hiyo na kutia saini.
(l) Kuhifadhi nakala za masharti haya, kanuni na sheria ya vyama vya
ushirika na nyaraka hizi ziwe wazi kukaguliwa na wanachama
wanapohitaji.
(m) Kufanya kazi nyingine zote ambazo atapewa / ataagizwa na bodi ya
uongozi.
13.2.6 KAZI ZA MWEKA HAZINA
TSACCOS itaajiri Mweka Hazina/Mhasibu mwenye sifa na ujuzi wa
kutosha. Aidha mwanachama mmojawapo mwenye ujuzi wa utunzaji
vitabu anaweza kufanya kazi ya Mweka Hazina na kulipwa ujira kidogo.
Kazi za Mweka Hazina zitakuwa hizi zifuatazo:-
(a) Kuandika na kutunza vitabu vya mahesabu na kumbukumbu nyingine
za fedha kwa kufuata kanuni za uandishi wa vitabu.
(b) Kutunza fedha na mali za TSACCOS kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
(c) Kupokea fedha yote iingiayo ndani ya TSACCOS na kufanya
malinganisho ya fedha iliyopokelewa na iliyolipwa kila siku.
(d) Kufanya malipo yote baada ya kupata kibali maalumu cha bodi ya
uongozi. Kamati ya mikopo au Afisa mikopo.
(e) Kukusanya marejesho ya mikopo na faida.
(f) Kufanya malinganisho ya hesabu ya benki kila mwezi.
(g) Kuyatayarisha orodha ya wadaiwa kila mwezi na kuwasilisha kwa bodi
ya uongozi na kamati ya mikopo ambao watatoa uamuzi kuhusu hatua
za kuwachukulia wanachama waliocheleweshwa madeni yao zaidi ya
miezi mitatu.
(h) Kusaidia wanachama katika kujaza fomu ya maombi ya mikopo na
kuziwasilisha kwa kamati ya mikopo ili zifikiriwe.
(i) Kuandaa taarifa ya kila mwezi ya hali ya fedha na takwimu (monthly
financial and statistical report form) na kuiwasilisha kwa bodi ya
uongozi na nakala kwa afisa ushirika wilaya, mkoani na Mrajis wa
vyama vya Ushirika.
(j) Kutia saini katika hundi za TSACCOS.
(k) Kusimamia shughuli zote za kila siku ndani ya TSACCOS zihusuzo fedha.
22
SEHEMU YA KUMI NA TATU
13.0 MIKUTANO MIKUU
Mkutano Mkuu ndiyo mwenye madaraka na mamlaka ya mwisho ya
uendeshaji wa shughuli za LAKWAO TSACCOS. LAKWAO TSACCOS
itakuwa na Mikutano Mikuu ifuatayo:-
(i) Mkutano Mkuu wa mwaka
(ii) Mkutano Mkuu wa kawaida
(iii) Mkutano Mkuu maalum
13.1 Mkutano Mkuu wa Mwaka
(a) Mkutano Mkuu wa mwaka wa TSACCOS utafanyika mara baada ya
kufunga mwaka wa fedha wa TSACCOS na isizidi miezi mitatu baada ya
mwisho wa mwaka wa hesabu.
(b) Mahudhurio ya Mkutano Mkuu yasipungue nusu (1/2) ya wanachama
wote au 100. Idadi isipotimia Mwenyekiti ataahirisha mkutano na
kupanga siku nyingine ya kufanya ndan ya siku 7 na idadi yoyote ya
wanachama waliohudhuria itafanya mkutano kuwa halali. Agenda ni
zile zile za mkutano ulioahirishwa.
(c) Mambo yafuatayo lazima yajadiliwe katika Mkutano Mkuu wa
Mwaka:-
(i) Kusoma na kuthibitisha mambo ya Mkutano Mkuu uliopita na
yatokanayo.
(ii) Taarifa za Mwenyekiti, Mweka Hazina na Katibu wa TSACCOS.
(iii) Kujadili taarifa ya ukaguzi wa Mrajis na kukubali au kukataa
taarifa ya mwaka ya mahesabu na mizania.
(iv) Kufanya uchaguzi wa wajumbe wa bodi na kamati mbalimbali za
TSACCOS ikibidi kusimamisha na kufukuza baadhi yao.
(v) Kujadili namna ya kugawana ziada kwa kuzingatia masharti ya
TSACCOS, kanuni na sheria ya vyama vya ushirika.
(vi) Kujadili mapendekezo ya miradi ya TSACCOS na kutoa
maamuzi.
(vii) Kuidhinisha ununuzi na uuzaji wa mali za TSACCOS zenye
thamani kama inavyoruhusiwa na sheria ya ushirika.
(viii) Kuzungumza mambo mengine yanayohusu maendeleo ya
TSACCOS kwa jumla na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa
bodi ya uongozi.
(ix) Kuidhinisha makisio ya mapato na matumizi ya mwaka
unaofuata.
(x) Kufikiria kiwango cha honoraria kwa ajili ya bodi ya uongozi.
(xi) Kuweka kiwango cha riba juu ya mikopo na amana za wasio
wanachama.
(xii) Kuweka idadi ya hisa na thamani ya hisa moja.
23
(xiii) Kubadili au kufanya marekebisho yoyote katika masharti haya
kama ilivyo kwenye sheria ya vyama vya ushirika NA. 20 ya
mwaka 2003 kifungu Na. 46.
(xiv) Kujadili mapendekezo ya sera za TSACCOS.
(xv) Kupokea na kuthibitisha maombi ya wanachama wapya na
wanaojitoa.
13.2 MIKUTANO MIKUU YA KAWAIDA
(a) Kutakuwepo na Mikutano Mikuu ya kawaida miwili ambayo itafanyika
wakati wowote katika mwaka wa fedha wa TSACCOS.
(b) Mambo yafuatayo yatajadiliwa katika Mkutano Mkuu wa kawaida:
(i) Kuthibitisha muhtasari wa mkutano uliopita na yatokanayo.
(ii) Kujadili na kufikiria taarifa za maendeleo ya utekelezaji kutoka
kwa bodi ya uongozi, kamati ya mikopo na ya usimamizi.
(iii) Kuthibitisha kuingizwa au kufukuzwa kwa wanachama.
(iv) Kuidhinisha makisio ya mapato na matumizi ya mwaka
unaofuata.
(v) Kuweka ukomo wa madeni kwa mujibu wa sheria ya vyama vya
ushirika.
(vi) Kuzungumzia mambo yote yanayohusu maendeleo ya TSACCOS
kwa jumla na kutoa maelekezo ya utekelezaji. Hata hivyo
wanachama waliohudhuria mkutano wowote wanaweza
kuamua kubadilisha kwa muda mambo yatakayozungumzwa
kwa kura ya 2/3 ya wajumbe wote.
13.3 MKUTANO MKUU MAALUM
Kutakuwepo na Mkutano Mkuu Maalum wakati wowote utakapohitajika
na utaitishwa na:-
a) Mrajis wa vyama vya ushirika au Afisa aliyeidhinishwa naye.
b) Kwa maombi ya maandishi ya wanachma wasiopungua theluthi moja
(1/3) ya wanachama wote. Maombi ya wanachma hao ni budi yataje
sababu au jambo/mambo yatakayozungumzwa na waombaji lazima
waweke saini zao au alama za dole gumba. Nakala ya maombi hayo
itapelekwa kwa Mrajis au mwakilishi wake.
Mkutano Mkuu Maalum ulioitishwa kwa mujibu wa kifungu cha 36 kanuni
za vyama vya ushirika za mwaka 2004 hautajadili mambo mengine zaidi
ya yale yaliyotakiwa. Mkutano Mkuu Maalum ulioitishwa na Mrajis
utaongozwa naye au mwakilishi wake.
13.4 KUITISHA MIKUTANO MIKUU
a) Matangazo ya Mikutano Mikuu yatabandikwa katika ofisi ya TSACCOS
na kwenye mbao za matangazo au kwa kutumia taratibu nyingine
zinazokubalika.
24
b) Muda wa matangazo ya Mikutano Mikuu kwa mujibu wa kanuni za
vyama vya ushirika za mwaka 2004 kifungu cha 37 ni kama ifuatavyo:-
(i) Mkutano Mkuu wa mwaka na si chini ya siku 21.
(ii) Mkutano Mkuu wa kawaida si chini ya siku 21.
(iii) Mkutano Mkuu maalum si chini ya siku 7.
13.5 AKIDI KATIKA MIKUTANO
Kwa mujibu wa kanuni za vyama vya ushirika za mwaka 2004 kifungu cha
38 mahudhurio ya lazima katika Mikutano Mikuu itakuwa:
(i) Mahudhurio ya lazima katika mikutano ya chama yatabidi kuwa si
chini ya nusu ya wanachama wote au asilimia (100) ukichukulia
idadi yoyote iliyo ndogo. Uwakilishi utakubalika kwa wanachama
nje ya Makao Makuu.
(ii) Kwa Mkutano Mkuu ulioitishwa na Mrajis au Afisa aliyeteuliwa na
Mrajis idadi yoyote ya wanachama waliohudhuria wataendesha
mkutano na yoyote yatakayozungumzwa yatakuwa ni halali.
(iii) Kwa Mikutano Mikuu ya Mwaka na Kawaida ikiwa mahudhurio ya
lazima hayatoshi baada ya saa moja na nusu ya saa zilizopangwa
kupita, mkutano utaahirishwa kwa siku saba (7), na mkutano
utakaofuata mambo yatakayozungumzwa ni yale yale ya mkutano
ulioahirishwa. Iwapo mahudhurio hayatatosha tena, wanachama
waliohudhuria wanaweza kuendesha mkutano na maazimio
yanaweza kutolewa na idadi isiyopungua nusu (1/2) ya wanachama
waliohudhuria na maamuzi yatakuwa halali.
(iv) Kwa Mkutano Mkuu Maalum ulioitishwa na wanachama, Mkutano
utafutwa kabisa iwapo mahudhurio hayatatosha.
(v) Mwenyekiti wa TSACCOS ataendesha Mikutano Mikuu yote
isipokuwa Mkutano Mkuu Maalum ulioitishwa na Mrajis ambapo
Mrajis mwenyewe au Afisa yeyote atakayemteua atakuwa
Mwenyekiti. Mwenyekiti akiwa hayupo makamu wake ataongoza
mkutano. Iwapo wote wawili hawapo au hawataki kusimamia
mkutano huo katika muda wa dakika 30 baada ya muda
uliopangwa kuanza mkutano kupita, mwanachama yeyote katika
waliohudhuria atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa muda na
ataongoza mkutano huo.
25
SEHEMU YA KUMI NA NNE
14.0 UIDHINISHAJI NA UWEKAJI SAINI KUMBUKUMBU ZA TSACCOS
Kumbukumbu zote na mikataba ya TSACCOS itasainiwa na Mwenyekiti, au
Makamu Mwenyekiti, kama Mwenyekiti hayupo. Katibu/Meneja na kama
Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hayupo basi mjumbe mmoja wa Bodi
ya uongozi.
SEHEMU YA KUMI NA TANO
15.0 UKOMO WA MADENI
Mkutano Mkuu wa TSACCOS lazima uweke ukomo wa madeni na ambao
utaidhinishwa na Mrajis msaidizi wa vyama vya Ushirika kama ilivyo
kwenye sheria ya ushirika.
SEHEMU YA KUMI NA SITA
16.0 MUHURI WA TSACCOS “COMMON SEAL”
(a) TSACCOS itakuwa na “Common Seal” na muhuri huo utakuwa na jina
kamili la chama LAKWAO TSACCOS LTD (LAKWAO Talanta Savings
and Credit Cooperative Society (2008) Ltd) na itakuwa tofauti na
mihuri ya kawaida ya TSACCOS.
(b) “Common Seal” itatunzwa ndani ya kasiki na kutumika na wahusika
wakuu tu wanao saini kumbukumbu za TSACCOS.
SEHEMU YA KUMI NA SABA
17.0 MAREKEBISHO YA MASHARTI
Masharti haya yatafanyiwa marekebisho kulingana na sheria ya ushirika na
marekebisho hayo hayatakuwa halali hadi hapo yatakapoidhinishwa na
kuandikishwa na Mrajis wa vyama vya ushirika.
SEHEMU YA KUMI NA NANE
18.0 KUVUNJWA AU KUFUTWA KWA TSACCOS
TSACCOS itaweza kuvunjwa na kufutwa kwa sababu zifuatazo:-
(a) Kwa maombi ya wanachama wasiopungua ¾ ya wanachama wote.
(b) Iwapo wanachama wamepungua na kuwa chini ya ishirini (20).
(c) Kwa amri ya Mrajis wa vyama vya ushirika chini ya kifungu 97 na 98
cha sheria ya vyama vya ushirika na 20 ya mwaka 2003.
26
SEHEMU YA KUMI NA TISA
19.0 MENGINEYO
(a) Migogoro au malalamiko yoyote kuhusu masharti au huduma za
TSACCOS kati ya wanachama au wanachama wa zamani au watu
wanaodai kupitia TSACCOS Bodi ya uongozi wa Afisa yeyote au kati
ya TSACCOS hii na Afisa yeyote, au kati ya TSACCOS na TSACCOS au
kati ya TSACCOS na chama kikuu (SCCULT) yapelekwe kwa Mrajis wa
vyama vya ushirika.
(b) Masharti haya yatasaidiwa na viambata au visaidizi kama vile kanuni za
fedha, kanuni za utumishi, sera na utaratibu za mikopo na kununi za
uhasibu.
19.1 Sisi tuliotia saini hapa chini ndiyo tulioteuliwa na mkutano wa
wanachama anzilishi wa LAKWAO TSACCOS (2008) LTD.
19.2 SAINI ZA WANACHAMA ISHIRINI (20)
NO JINA UMRI JINSI MAHALI WILAYA SAHIHI
1 PIUS MAJENGO
2 AUGUSTIN MOYA
3 HUSEIN YUSUFU
4 ZACHARIA SHIGUKULU
5 THEONIS NTWANGA
6 VICENT TARIMO
7 MALISELINA NCHIMBI
8 MATILDA NAMU
9 ISAYA MBUA
10 EMMANUEL JUMA
11 VIRGIN NJIKU
12 MWAJABU KITIMA
13 STELLA LAURENT
14 RAMADHAN ISSA
15 ROZI MAXIM
16 WILLIUM WENGA
17 BONIPHAS LOLA
18 OMARY ISSA
19 MARTIN DOMINIC
20 ELIZABETH MOYA
27
19.3 MUUNDO WA UONGOZI WA LAKWAO
TSACCOS(2008) LTD.