Tuesday, May 12, 2009

SERA YA AKIBA NA AMANA LAKWAO TSACCOS

1
Namba ya kuandikishwa . ……………………
SERA YA AKIBA NA AMANA
YA
CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO
CHA
LAKWAO TALANTA
SAVINGS AND CREDIT COOPERATIVE SOCIETY (2008) LTD.
LALTA
OVADA KWAMTORO
2
YALIYOMO
YALIYOMO ......................................................................................................................... 2
SERA YA AKIBA NA AMANA ............................................................................................ 3
UTANGULIZI .................................................................................................................. 3
DIRA YA CHAMA ........................................................................................................... 3
AZMA/MWELEKEO WA CHAMA .................................................................................. 3
MIPANGO YA MBELENI ................................................................................................ 3
MADHUMUNI YA CHAMA ............................................................................................. 3
SEHEMU YA 1 .................................................................................................................... 4
VYANZO VYA FEDHA ZA CHAMA ............................................................................... 4
SEHEMU YA II .................................................................................................................... 5
AINA ZA AKAUNTI ZA AKIBA NA AMANA ................................................................. 5
SEHEMU YA III ................................................................................................................... 5
UTARATIBU WA KUPOKEA AKIBA NA AMANA ........................................................ 5
a) Akiba na amana za wanachama .................................................................. 5
SEHEMU YA IV................................................................................................................... 6
AKIBA NA AMANA KUTUMIKA KAMA KIGEZO NA DHAMANA YA MIKOPO ......... 6
SEHEMU YA V .................................................................................................................... 6
MUDA WA KUWEKA AKIBA NA AMANA .................................................................... 6
SEHEMU YA VI................................................................................................................... 7
KUCHUKUA NA KUREJESHA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA ................... 7
SEHEMU YA VII ................................................................................................................. 7
USALAMA WA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA ............................................ 7
SEHEMU YA VIII ................................................................................................................ 8
RIBA JUU YA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA ............................................. 8
3
SERA YA AKIBA NA AMANA
LAKWAO T SACCOS(2008) LTD
UTANGULIZI
Sera ya akiba na amana ni mwongozo ulioandaliwa na chama cha ushirika wa
Akiba na mikopo (LAKWAO T SACCOS LTD) kwa ajili ya uwekaji akiba na amana
za wanachama na wateja wake.
Talanta chama cha ushirika cha Akiba na mikopo (LAKWAO T SACCOS LTD) ni
asasi ya hiari ya kifedha inayowahudumia wanachama na wateja
wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi katika tarafa ya
Kwamtoro. Makao makuu ya chama yapo katika kijiji cha Ovada.
LAKWAO T SACCOS LTD imeandikishwa kama chama cha ushirika wa akiba na
mikopo chini ya sheria ya ushirika na. 20 ya mwaka 2003 na imeandikishwa kwa
Na ………………………...
DIRA YA CHAMA
Asasi ya kifedha inayoongoza katika utoaji wa huduma bora za kifedha vijijini
kwa kushirikisha wadau wote.
AZMA/MWELEKEO WA CHAMA
Kuwawezesha wanachama wengi kununua hisa, kuweka akiba na amana ili
kupata mikopo yenye masharti na gharama nafuu ili kujieletea maendeleo
endelevu.
MIPANGO YA MBELENI
a) kuhamasisha na kuelimisha jamii kujiunga na LAKWAO T SACCOS LTD
b) kushirikiana na asasi nyingine za kifedha za ndani na nje ya nchi
c) kuajiri watumishi wenye uelewa pevu juu ya ushirika wa akiba na mikopo
ili watoe huduma bora na endelevu kwa wanachama na wasio
wanachama.
MADHUMUNI YA CHAMA
Madhumuni ya LAKWAO T SACCOS LTD pamoja na mambo mengine ni:-
(a) kuendeleza uanachama wa mtu mmoja mmoja na kukuza uwezo wao
kiuchumi ili kuwawezesha kujiwekea akiba, kukopa kwa ajili ya shughuli
za kiuchumi na kurejesha kwa wakati kupitia vikundi vyao vya
wanachama 10-15.
(b) Kupokea kiingilio, hisa, akiba na amana kutoka kwa wanachama na
kutoa mikopo kwa kuzingatia kiwango cha akiba na amana za
mwanachama.
(c) Kujenga tabia ya kujiwekea akiba na amana na kuepuka matumizi
yasiyo ya lazima miongoni mwa wanachama.
4
(d) Kuweka viwango vya riba juu ya akiba, amana na mikopo kwa
wanachama dhidi ya hasara/majanga.
(e) Kuunda mtaji wa kutosha kuendesha shughuli za LAKWAO T SACCOS
LTD.
(f) Kujenga na kuimarisha uwezo wa wanachama kuendesha na kusimamia
chama kwa njia ya elimu ya ushirika na ushirikishwaji wa wanachama.
(g) Kubuni utaratibu mzuri wa kutoa taarifa za shughuli za LAKWAO T
SACCOS LTD kwa wanachama na kupokea maombi ya wanachama
wapya.
(h) Kununua hisa na dhamana (bond) kwenye vyombo vya fedha na serikali
baada ya kufanya utafiti wa kina wa kitaalamu.
(i) Kuwawezesha wanachama kuongeza kipato katika kaya na kusaidia
kuongeza mzunguko wa fedha katika eneo lao kwa kuhakikisha kuwa
huduma na mahitaji muhimu yanapatikana kwa urahisi katika eneo la
LAKWAO T SACCOS LTD.
(j) Kutoa elimu ya ujasiriamali na uendeshaji na usimamizi wa biashara
kwa wanachama.
(k) Kushirikiana na taasisi nyingine za fedha na vyama vingine vya akiba na
mikopo kwa ajili kuongeza mtaji wa chama cha kusaidiana.
(l) Kufanya shughuli nyingine muhimu kwa manufaa ya wanachama na
ustawi wa LAKWAO T SACCOS LTD.
SEHEMU YA 1
VYANZO VYA FEDHA ZA CHAMA
LAKWAO T SACCOS LTD inatarajia kupata fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli
zake, kuwekeza kwenye vitega uchumi na kutoa mikopo kwa wanachama
kutoka vyanzo vifuatavyo:-
a) Viingilio vya wanachama
b) Hisa za wanachama
c) Akiba za wanachama
d) Amana za wanachama na wateja
e) Faida kutoka Benki
f) Mikopo kutoka taasisi zingine
g) Adhabu/faini
h) Misaada au zawadi au ruzuku
i) Akiba na malimbikizo ya lazima
j) Faida kutoka vitega uchumi kama vile gawiwo (dividend) kutoka
makampuni mbalimbali ambako LAKWAO T SACCOS LTD imenunua
hisa/imewekeza.
k) Riba kutoka mikopo ya wanachama
l) Riba zitokanazo na kuhifadhi amana za wateja
m) Viingilio vya wanachama
5
SEHEMU YA II
AINA ZA AKAUNTI ZA AKIBA NA AMANA
LAKWAO T SACCOS LTD itaendesha aina tofauti za akaunti ya akiba na amana
kama ifuatavyo:-
a) Akaunti za akiba
i) Akaunti ya akiba ya lazima kwa ajili ya kujenga fungu la
kukopeshana.
ii) Akaunti ya akiba kwa ajili ya elimu ya watoto
b) Akaunti za amana
i) Akaunti ya amana ya kawaida kwa ajili ya matumizi ya kila siku
ya mwanachama au mteja
ii) Akaunti ya amana ya muda maalum (muda unaweza ukawa ni
wa miezi kadhaa (sita) au miaka kadhaa (mf. Miwili)
SEHEMU YA III
UTARATIBU WA KUPOKEA AKIBA NA AMANA
a) Akiba na amana za wanachama
i.) kuweka akiba katika LAKWAO T SACCOS LTD ni jambo la lazima
kwa kila mwanachama. Kila mwanachama wa LAKWAO T SACCOS
LTD ni lazima ajenge tabia ya kuweka akiba mara kwa mara ili
kujenga fungu la kukopeshana kama ilivyo katika masharti.
ii.) Mwanachama anaweza kuweka amana katika LAKWAO T SACCOS
LTD.
iii.) Akiba na amana zitalipwa kwa fedha taslimu tu na sio vinginevyo
iv.) Fedha za mwanachama zinaweza kupelekwa/kuwekwa na mwenye
akaunti yeye mwenyewe au mweka hazina wa kikundi chake au
kiongozi yeyote wa kikundi chake au mtu yeyote atakeyekuwa
ameaminiwa na mwenye fedha.
v.) Mweka hazina wa LAKWAO T SACCOS LTD ni lazima aandike
stakabadhi ya fedha mara tu akishapokea fedha za mwanachama
akifuatiwa na maingizo katika vitabu na kumbukumbu nyingine za
fedha kulingana na mfumo wa uhasibu uliopo.
b) Amana za wateja
Wasio wanachama (wateja) wanaweza kuweka amana zao katika
LAKWAO T SACCOS LTD kwa kulipia gharama kidogo. LAKWAO T SACCOS
LTD inaweza kupokea amana kutoka kwa makundi mbalimbali kama
vile:-
6
i) Wafanyabiashara wanaokuja kununua mifugo au mazao kwa
kuhifadhi fedha zao na kuchukua kidogo kidogo kulingana na
mahitaji yao ya kibiashara
ii) Taasisi zinazokuja kuendesha mafunzo au semina wanaweza
kuhifadhi fedha zao kwa usalama kwa muda katika chama.
iii) Wananchi wa kawaida na/ au taasisi zilizomo ndani na/au nje
ya eneo la chama.
Mteja anayekuja kuweka fedha zake katika LAKWAO T SACCOS LTD atatozwa
ada ya asilimia moja (1%) ya kiasi cha fedha kilichowekwa kwa kipindi cha
mwezi mmoja. Baada ya muda/kipindi hicho kupita ada yake itakuwa nusu ya
asilimia (0.5%) ya kiasi cha fedha kilichobaki.
SEHEMU YA IV
AKIBA NA AMANA KUTUMIKA KAMA KIGEZO NA DHAMANA YA MIKOPO
a.) Akiba na Amana za wanachama wa LAKWAO T SACCOS LTD zitatumika
kama kigezo na dhamana ya mikopo.
b.) Mwanachama ataruhusiwa kukopa mara mbili ya kiasi cha akiba na
amana alizonazo chamani wakati wa kuomba mkopo.
c.) Amana za mwanachama zinapotumika kama dhamana ya mkopo
hazitaruhusiwa kuchukuliwa hadi pale mkopaji atakaporejesha mkopo
aliopewa pamoja na riba yake.
d.) Kiasi chochote cha akiba na amana alizonazo mwanachama
kitamwezesha kuomba mkopo.
SEHEMU YA V
MUDA WA KUWEKA AKIBA NA AMANA
a.) Mwanachama wa LAKWAO T SACCOS LTD ataweka akiba na amana wakati
wowote wa mwaka kulingana na hali ya mapato.
b.) Mwanachama ataweka kiasi chochote kile kwenye akaunti yake ya akiba.
Hata hivyo mwanachama anashauriwa kuweka kiasi kisichopungua
asilimia kumi (10%) ya mapato yake anayopata kwa vipindi tofauti.
7
SEHEMU YA VI
KUCHUKUA NA KUREJESHA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA
Mwanachama wa LAKWAO T SACCOS LTD atarejeshewa au kuchukua akiba zake
endapo:-
a) Ataamua kujitoa
b) Atahama eneo la chama
c) Atafukuzwa uanachama
d) Atathibitika kuwa ni mwenda wazimu (mwanachama aliyepata na
kuthibitika kuwa ni mwendawazimu anaweza kurejeshewa haki zake au
kukabidhiwa kwa mtu yeyote atakayeteuliwa naye kumiliki haki zake
kwa niaba yake).
e) Atafariki dunia (mwanachama anapofariki dunia haki zake zote
zitahamishiwa kwa mrithi wake au kama aliweza kutoa maagizo yoyote
yatafuatwa).
f) Kupata ulemavu wa kudumu (kwa mwenye ulemavu wa kudumu hisa na
akiba zake zitaweza kurejeshwa kwa kulingana na aina ya ulemavu au
uamuzi wake mwenyewe).
Amana za mwanachama wa LAKWAO T SACCOS LTD zinaweza kuchukuliwa
wakati wowote ule kulingana na masharti ya chama. Mwanachama aliyepoteza
sifa za uanachama anaweza kuweka amana katika chama.
SEHEMU YA VII
USALAMA WA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA
Ili kuhakikisha kuwa fedha za wanachama na wateja wa LAKWAO T SACCOS LTD
zinakuwa salama mambo yafuatayo yatazingatiwa:-
a) Fedha zote zitapokelewa na mwenye mamalaka ya kupokea fedha kwa
niaba ya chama (mweka hazina)
b) Chama kitaajiri mweka hazina mwenye ujuzi na uaminifu wa hali ya juu
c) Ofisi ya chama italindwa na mlinzi mwenye silaha ya masafa ya mbali
d) Fedha zitawekewa bima
e) Fedha zitahifadhiwa katika benki ya CRDB isipokuwa kiwango/kiasi
kidogo kwa matumizi ya dharura.
f) Ofisi ya chama itakuwa kwenye jengo imara na la kudumu
g) Kutakuwa na kasiki kwa ajili ya kutunzia kiasi kidogo cha fedha
h) Kiasi cha fedha cha chini kabisa kitakachotunzwa katika kasiki kwa
matumizi ya dharura kitakuwa Tshs. 500,000/=
8
SEHEMU YA VIII
RIBA JUU YA AKIBA NA AMANA ZA MWANACHAMA
LAKWAO T SACCOS LTD inaweza kutoa riba/faida juu ya akiba na amana za
mwanachama. Riba inayoweza kutolewa kwa ajili ya akiba na amana
zilizowekwa na wanachama itakuwa pungufu kwa asilimia moja (1%) ya ile
(riba) inayotolewa na benki ya NMB/CRDB kwa mwaka.

No comments: